Wilaya ya Kilombero inatokana na jina la mto mkubwa katika mkoa wa Morogoro uliopo kusini magharibi mwa Tanzania. Wilaya ipo kati ya mto Kilombero ambao unapatikana kusini mashariki na milima udzungwa ambayo ipo kaskazini magharibi , kwa upande mwingine kusini mashariki mwa mto kilombero wilaya inapakana na wilaya ya ulanga.
Wilaya ya Kilombero ni mojawapo ya wilaya saba za Mkoa wa Morogoro ambazo ni Morogoro Manispaa, Morogoro vijijini, Gairo, Mvomero, Kilosa na Ulanga .
Wilaya ya Kilombero iko upande wa magharibi wa Mkoa wa Morogoro. wilaya iko kati ya latitudo 70° 40 'na 90°21' kusini mwa Ikweta na kati ya longitudo 35°20 'na 37°48' mashariki ya longitudo 0.
Kaskazini mashariki wilaya ya Kilombero inapakana na wilaya za Kilosa na Morogoro vijijini na upande wa Kusini magharibi Kilombero inapakana na wilaya ya Mufindi na Njombe, upande wa kaskazini wilaya ya Kilombero inapakana na wilaya ya Kilolo ambayo ipo mkoani Iringa.
Kusini mashariki mwa mto Kilombero wilaya hii inapakana na wilaya ya Ulanga na upande wa kusini wilaya ya Kilombero inapakana na wilaya ya Songea vijijini iliyoko mkoa wa Ruvuma.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa