Leseni za biashara zinatolewa katika ofisi za biashara zilizopo makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, ili upate leseni unatakiwa uwe teyali umeshalipia kodi ya mapato katika ofisi za mapato (TRA) , kisha unakuja katika ofisi zetu ambapo utasajiliwa kwenye mfumo wa mapato wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero kwa taarifa zako kuhusiana na aina ya biashara unayofanya.
Usajili wako utakapokamilika utapatiwa hati ya malipo ya leseni ya biashara ambayo utakwenda kuilipa katika benki ya NMB iliyo karibu nawe kupitia akaunti iliyoainishwa kwenye hati yako ya malipo, mara baada ya malipo kukamilika benk utatakiwa kurudi katika ofisi za biashara ukiwa na nakala ya malipo kutoka benk ili uweze kupatiwa leseni yako.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa