• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MLIMBA DISTRICT COUNCIL
MLIMBA DISTRICT COUNCIL

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA MLIMBA

  • Mwanzo
  • kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/ Asili
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
      • Muonekano wa muundo
    • Idara/ Vitengo
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Miundombinu
      • Fedha na Biashara
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango, Takwimu na ushirika
      • Mazingira na Usafi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Maji
      • Ardhi, Maliasili na Mazingira
      • Ufugaji na uvuvi
      • CHF iliyoboreshwa
      • Sheria
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Msingi
      • Sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za watumishi
    • Rasilimali watu
    • TEHAMA
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha, utawala na mipango
      • Elimu, Afya na maji
      • Uchumi, Ujenzi na mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Kumuona mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
      • PICHA ZA MIRADI YA MAPAMBANO DHINI YA UVICO

HALMASHAURI YA MLIMBA YAKEMEA UCHIMBAJI HOLELA WA VIFUSI NA UHARIBIFU WA MTO MNGETA, YAAHIDI KUDHIBITI NYANI WAHARIBIFU KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA KIBURUBUTU

Posted on: January 19th, 2026

Na; Milka Kaswamila-Afisa Habari-Mlimba DC

Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira cha Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, kimekemea vikali uchimbaji holela wa vifusi, uharibifu wa mto Mngeta pamoja na kuahidi kudhibiti nyani waharibifu katika Shule ya Sekondari Kiburubutu, iliyopo Kata ya Mngeta.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo hicho, Ndg. Jaji Mafuru Machumu, alipokuwa akiongoza timu ya wataalamu kutoka sekta za mazingira, misitu na nyuki katika ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku, iliyohusisha mto Mngeta, Shule ya Sekondari Kiburubutu na eneo ambalo wananchi wameanza kuchimba vifusi kiholela katika Kijiji cha Kidete, karibu na Shule ya Sekondari Mchombe.

Akiwa Kijiji cha Kidete, Ndg. Mafuru amesema wataalamu hao wamebaini uwepo wa shimo la kifusi lililochimbwa kiholela na wananchi binafsi ndani ya umbali wa mita 60 kutoka reli ya TAZARA, hali inayoweza kusababisha mmomonyoko wa udongo, kuhatarisha usalama wa reli hiyo pamoja na kuharibu mazingira kwa ujumla.

Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba, amewataka wananchi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchimbaji wa vifusi, ikiwemo kupata vibali halali kutoka Ofisi ya Kijiji husika, ambako Mtendaji wa Kijiji ndiye mwenye mamlaka ya kutoa vibali hivyo.

Katika Shule ya Sekondari Kiburubutu, wataalamu hao walioneshwa maeneo ambayo nyani huvamia na kusababisha usumbufu shuleni, ambapo wameahidi kuandaa mikakati ya muda mfupi na mrefu ya kudhibiti tatizo hilo.

Wakati wa ziara yao katika mto Mngeta, ambao ni mojawapo ya vyanzo muhimu vya maji kwa mto Kilombero, wataalamu hao walibaini kuwa shughuli za kilimo na usafirishaji zinafanyika ndani ya mita 60 kutoka kingo za mto, hali inayochangia uharibifu wa mazingira ya mto huo. Kutokana na hali hiyo, wameazimia kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa misitu kwa wananchi wa vijiji vya Mngeta na Itongowa ili kuhakikisha misitu inaendelea kulindwa na vyanzo vya maji vinahifadhiwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Awali, kabla ya kufika mto Mngeta, timu hiyo ilitembelea Ofisi za SUMA JKT (KPL) kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili namna bora ya kushirikiana katika uhifadhi wa misitu inayozunguka mto Mngeta na kuudhibiti uharibifu wa mazingira ya mto huo, ikiwemo kudhibiti shughuli za kilimo kandokando ya mto huo, kutokana na umuhimu wake kwa shughuli za shirika hilo zikiwemo uzalishaji wa umeme.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA DARASA LA SABA MWAKA 2025 November 05, 2025
  • MATOKEO YA USAILI WA MAANDISHI WA MAAFISA UGANI KWA AJILI YA MRADI WA MIFUMO YA CHAKULA, MARUMIZI YA ARDHI NA UREJESHAJI WA MAZINGIRA (FOLUR) KATIKA HALMASHAURI YA MLIMBA December 06, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA MLIMBA YAPOKEA WAAJIRIWA 118

    January 20, 2026
  • HALMASHAURI YA MLIMBA YAKEMEA UCHIMBAJI HOLELA WA VIFUSI NA UHARIBIFU WA MTO MNGETA, YAAHIDI KUDHIBITI NYANI WAHARIBIFU KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA KIBURUBUTU

    January 19, 2026
  • MRADI WA FOLUR KUANZA KUTEKELEZWA KWA VITENDO

    January 18, 2026
  • HALMASHAURI YA WILAYA MLIMBA IMEFANYA MKUTANO WA ROBO YA PILI, WA BARAZA LA MADIWANI

    January 18, 2026
  • Angalia zote

Video

Kupata Madarakani au cheo hakukufanyi kujua kila kitu. Maneno ya hekima kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu Mhe. Mhe. Dkt Doto Biteko
video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Fomu ya maombi ya ruhusa
  • Fomu ya utambulisho benki
  • Fomu ya Kuhuisha Uanachama CHF iliyoboreshwa
  • Wasifu wa Wilaya
  • Muundo wa Halmashauri
  • Eneo la Kijiografia
  • Fursa za Uwekezaji Kilombero

Viunganishi linganifu

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Idara kuu ya Takwimu (NBS)
  • TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

kitafutio cha watembeleaji wa duniani

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Mngeta Kijiji cha Itongoa

    Anuani: P.O.BOX 263

    Simu: 023 293 1523

    Mobile: 0232931523

    Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa