Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ilianzishwa rasmi tarehe 5 Mei, 2020 kupitia cheti cha kuanzishwa na GN 305A chini ya masharti ya vifungu vya 7, 9, 10, 11 na 12 vya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), 1982. Halmashauri hii ni matokeo ya kubadilika kwa eneo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero ya zamani na hivyo kuunda Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba na Halmashauri ya Mji Ifakara.
Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba ni mojawapo ya halmashauri 9 za wilaya katika Mkoa wa Morogoro, halmashauri nyingine ni Malinyi, Ulanga, Ifakara, Manispaa ya Morogoro, Morogoro DC, Kilosa, Mvomero na Gairo.
Ofisi ya Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya Mlimba ipo katika kijiji cha Itongowa, kata ya Mngeta, umbali wa km320 kutoka makao makuu ya mkoa wa Mororogoro, na kwa upande wa mipaka, inapakana na Mji wa Ifakara na Manispaa ya Morogoro upande wa Kaskazini Mashariki, Wilaya ya Mufindi na Njombe upande wa Kusini na Kusini Magharibi inapakana na Wilaya ya Kilolo upande wa Kaskazini, na Wilaya ya Malinyi upande wa Kusini Mashariki.
Kiutawala, Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba inazo tarafa 2 (Mngeta,a Mlimba), kata 16, vijiji 62 na vitongoji 244.
Kulingana na Kifungu cha 148 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) ya 1982, Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kama mamlaka nyingine za serikali za mitaa ina jukumu la kutekeleza majukumu makuu matatu ambayo ni:-
i. Kudumisha sheria, amani na utawala bora;
ii. Kukuza ustawi wa kiuchumi na kijamii wa watu katika eneo lake la utawala;
iii. Kuhakikisha utoaji bora na sawa wa huduma za ubora na idadi kwa watu ndani ya maeneo yake ya utawala.
Mbali na majukumu hayo ya msingi, kulingana na Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, 1982, Halmashauri ya Mlimba kama zilivyo serikali za mitaa zingine, ina majukumu mengine kama ifuatavyo:
Kuunda, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa mipango yote ya maendeleo ya kiuchumi, viwanda na kijamii katika maeneo yao ya utawala.
ii. Kufuatilia na kudhibiti utendaji wa majukumu na kazi za halmashauri na wafanyakazi wake.
iii. Kuhakikisha ukusanyaji na matumizi sahihi ya mapato ya halmashauri.
iv. Kutunga kanuni zinazotumika katika maeneo yote ya utawala wake, na kuzingatia na kuboresha kanuni zinazotungwa na halmashauri za vijiji ndani ya maeneo yake ya utawala.
v. Kuhakikisha, kudhibiti na kuratibu mipango ya maendeleo, miradi na programu za halmashauri za vijiji na miji ndani ya maeneo yake ya utawala.
vi. Kudhibiti na kufuatilia ukusanyaji na matumizi ya mapato ya halmashauri za vijiji na miji.
vii. Kulingana na sheria zilizopo, kufanya vitendo vyote na mambo yote yanayoweza kufanywa na serikali ya watu.
viii. Kutunga kanuni zinazotumika katika maeneo yote ya utawala wake, na kuzingatia na kuboresha kanuni zinazotungwa na halmashauri za vijiji ndani ya maeneo yake ya utawala.
ix. Kuhakikisha, kudhibiti na kuratibu mipango ya maendeleo, miradi na programu za halmashauri za vijiji na miji ndani ya maeneo yake ya utawala.
x. Kudhibiti na kufuatilia ukusanyaji na matumizi ya mapato ya halmashauri za vijiji na miji.
xi. Kulingana na sheria zilizopo, kufanya vitendo vyote na mambo yote yanayoweza kufanywa na serikali ya watu.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa