MAJUKUMU YA NGAZI YA UTAWALA
i. Kusimamia sera na miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Kumshauri na kutolea ufafanuzi masuala yote ya kitaalam yanayohusu Idara ya Afya
ii. Kusimamia vituo vyote vya kutolea huduma za Afya ili vitoe huduma bora zinazoendana na viwango
iii. Kufanya ziara elekezi katika vituo vya kutolea huduma ili kutoa ushauri na kubaini changamoto mbali mbali zilizopo na kutafuta njia za kutatua changamoto hizo.
iv. Kupokea maagizo mbalimbali toka ngazi za juu na kuyafanyia kazi kisha kutoa mrejesho.
MAJUKUMU YA NGAZI YA VITUO VYA AFYA
i. Kutoa huduma za wagonjwa wa nje
ii. Kutoa huduma za maabara
iii. Kutoa huduma za upasuaji mdogo na wa dharura kwa mama wajawazito
iv. Kutoa huduma za wagonjwa wa ndani
v. Kutoa Huduma za Afya ya uzazi
vi. Huduma za kinga kwa magonjwa yanayoweza kukingwa
vii. Huduma za ustawi wa jamii zikiwemo huduma kwa wazee
viii. Kutoa huduma za Tiba,matunzo na Ushauri nasaha
ix. Kushiriki na wananchi katika kutekeleza shughuli za Afya
x. Kutoa rufaa kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za kitaalam zaidi
MAJUKUMU YA NGAZI YA ZAHANATI
i. Kutoa huduma za wagonjwa wa nje
ii. Kuta huduma za maabara
iii. Kutoa Huduma za Afya ya uzazi
iv. Huduma za kinga kwa magonjwa yanayoweza kukingwa
v. Kushiriki na wananchi katika kutekeleza shughuli za Afya
vi. Kutoa rufaa kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za kitaalam zaidi
MAJUKUMU YA NGAZI YA JAMII
i. Kuhamasisha jamii katika masuala mbalimbali yanayohusu afya mfano chanjo,uzazi wa mpango,michango ya CHF
ii. Kuhamasisha wananchi kuhusu maradhi yanayoweza kuzuilika, ili waweze kuyatambua na kutafuta mbinu za kuyadhibiti.
iii. Uibuaji wa miradi mbalimbali ya afya katika ngazi ya jamii
iv. Kutoa taarifa za vifo vinavyotokea kwenye jamii.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa