KITENGO CHA MKAGUZI WA NDANI
HISTORIA FUPI:
Kitengo cha Mkaguzi wa ndani wa Hesabu (Internal Audit Unit) kilianzishwa mwaka 2004 ikiwa
ni moja ya Mkakati wa maboresho katika Usimamizi wa Fedha katika Serikali za Mitaa.
MAJUKUMU YA IDARA:
• Kuandaa mpango kazi wa mwaka na kuuwasilisha kwa Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu
na Kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
• Kuandaa mpango wa ukaguzi unaozingatia majanga.
• Kupitia na kutoa taarifa juu ya udhibiti wa stakabadhi na utunzaji na matumizi ya
rasilimali za Halmashauri.
• Kupitia na kutoa taarifa juu ya sheria na kanuni za fedha kama zimekidhi maelekezo na
mfumo mzuri wa kihasibu.
• Kupitia na kutoa taarifa juu ya unyambulishaji na mgawanyo wa mapato na matumizi.
• Kupitia na kutoa taarifa juu ya takwimu za kifedha kuhakikisha taarifa sahihi za fedha na
taarifa nyingine zinaweza kutumiwa.
• Kutoa ushauri kuhusu mifumo mbalimbali iliyopo katika Halmashauri.
MIKAKATI YA IDARA:
• Kuhakikisha kwamba mfumo wa udhibiti wa ndani unaimarishwa.
MAFANIKIO YA KITENGO:
• Tangu kuanzishwa kwa kitengo cha Mkaguzi wa ndani Halmashauri ilikidhi vigezo vya
kupewa ruzuku ya maendeleo kutoka Serikali kuu kuanzia mwaka 2006
• Halmashauri imefanikiwa kupata hati safi mfululizo kwa zaidi ya miaka mitano.
• Kupitia kitengo cha Mkaguzi wa ndani,Halmashauri imefanikiwa kuweka mfumo mzuri
wa utoaji taarifa wa fedha za uchangiaji wa huduma ya afya(cost sharing)
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa