Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya vipatavyo 59 (Hospitali 1, Vituo vya afya 6 na zahanati 52). Miongoni mwa hivyo vituo vinavyomilikiwa na serikali ni vituo vya afya 4 na zahanati 22.
Idara ya Afya inatekeleza majukumu yake mbalimbali kwa kuzingatia sera na muundo wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto. Vile vile majukumu ya idara yanatekelezwa kulingana na ngazi tofauti za kiutawala katika idara. Ngazi hizo za kiutawala ni kama ifuatavyo;
i. Ngazi ya Utawala(CHMT)
ii. Ngazi ya Vituo vya Afya
iii. Ngazi ya Zahanati
iv. Ngazi ya jamii
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa