HIFADHI YATAIFA YA MILIMA YA UDZUNGWA
Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ni Hifadhi katika Tanzania ambayo ina wanyama (Mbega Wekundu) ambao hawapatikani katika asehemu yoyote Duniani. Pia ina mimea ambayo haipatikani katika sehemu yoyote dunuani isipokuwa katika hifadhi hii pekee. Vivutio vingine ni Maporomoko ya Sanje, Nyani waitwao Sanje Mangabay, Kilele cha Mlima Bokela na wanyama wengine wengi.
VYURA WA KIHANSI (KIHANSI SPRAY TOAD)
Vyura wa Kihansi waligunduliwa mwaka 1996 wakati wa zoezi la tathmini ya athari za Kimazingira wakati Ujenzi wa Mgodi wa kufua Umeme wa maji katika Mto Kihansi. Uvumbuzi wa vyura hawa mwanzoni ilifikiriwa kuwa ni jambo la kawaida na ujenzi wa mradi wa umeme ulidhaniwa kuwa hautakuwa na athari kubwa kwa vyura. Hata hivyo baada ya mgodi huo kuanza kazi mazingira na makazi ya asili ya vyura hao yalibadilika na idadi ya vyura hao ilianza kupungua kwa kasi. Hivi sasa inasadikiwa kuwa vyura hao wametoweka katika bonde la Mto Kihansi na waliochukuliwa ili kunusuru uhai wao bado wanatunzwa katika Bustani ya wanyama ya Toledo na Bronx huko Marekani. Aidha kwa sasa mazingira yanaandaliwa katika Bonde la Kihansi ili vyura hao waweze kurejeshwa katika makazi yao ya asili.
BONDE LA MTO KILOMBERO
Wilaya ya Kilombero iko ndani ya Bonde la Mto Kilombero na sehemu nyingine katika mbuga ya wanyama ya Selous. Bonde la Mto Kilombero ni maarufu kwa shughuli za uvuvi na uwindaji wa kitalii. Pia kuna ndege wanaoitwa Kilombero Weever Bird ambao wanapatikana katika Wilaya ya Kilombero pekee hususan katika Bonde la Mto Kilombero.
Maeneo mengine ya vivutio ni yale yaliyoko katika Mbuga ya wanyama ya Selous kama vile maajabu ya eneo linaloitwa Boma Ulanga, Stiglers Gorge katika Mto Kilombero.
MSITU WA HIFADHI ASILIA WA KILOMBERO
Hivi karibuni Wizara ya Maliasili na Utalii iliipandisha hadhi Misitu ya Hifadhi ya Kilombero Magharibi, Iyondo na Matundu kuwa Msitu wa Mazingira Asilia ya Kilombero na kuutangaza kuwa Eneo la Urithi wa Dunia katika Milima ya Tao la Mashariki.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa