DIVISHENI YA RASILIMALI WATU NA UTAWALA
Lengo
Kutoa utaalamu na huduma kuhusu usimamizi wa rasilimali watu na masuala ya kiutawala kwa Halmashauri na kuratibu masuala yote yanayo husu chaguzi kuu na za Serikali za Mitaa ndani ya Manispaa.
Majukumu
Divisheni hii inatekeleza majukumu yafuatayo:-
Kufafanua kanuni za huduma ya umma; kanuni za kudumu na sheria zingine za kazi;
Kusimamia utekelezaji wa shughuli za uhamasishaji wa maadili ikiwa ni pamoja na elimu ya kuzuia rushwa;
Kutoa na kusimamia utekelezaji wa shughuli kama vile kuajiri, kuchagua, kutoa mwelekeo, mafunzo na maendeleo ya mwajiriwa, kupandishwa vyeo, nidhamu, hamasa, uhifadhi, usimamizi wa utendaji na ustawi wa jumla wa wafanyakazi;
Kuhakikisha usimamizi bora na wa ufanisi na matumizi ya rasilimali watu;
Kuratibu Baraza la Wafanyakazi na masuala ya vyama vya wafanyakazi;
Kusimamia maendeleo na utekelezaji wa sera bora, taratibu na miongozo ya kuajiri, mafunzo na maendeleo, usambazaji na uhifadhi wa wafanyakazi, kupanda vyeo na usimamizi wa utendaji;
Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa rasilimali watu na orodha ya ujuzi wa sasa na unao hitajika;
Kutoa huduma za kumbukumbu, umesenja na uwakala; na kusimamia kumbukumbu za Ofisi;
Kusimamia masuala ya itifaki;
Kuwezesha utoaji wa huduma za usalama, usafiri na mahitaji ya jumla;
Kuwezesha ukarabati wa vifaa vya Ofisi, majengo na viwanja;
Kuratibu utekelezaji wa masuala mbalimbali;
Kuratibu utekelezaji wa Ushiriki wa Sekta Binafsi, uboreshaji wa Mchakato wa Biashara na Mkataba wa Huduma kwa Wateja;
Kutoa ushauri kuhusu ufanisi wa Taasisi ya Ofisi;
Kuratibu shughuli za uchaguzi kwenye Halmashauri; na
Kusimama chaguzi kuu na za Serikali za Mitaa.
Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimali Watu
Sehemu hii inatekeleza shughuli zifuatazo:-
Kutafsiri na kuhakikisha kanuni za huduma ya umma, kanuni za kudumu na sheria zingine za kazi zinafuatwa;
Kutekeleza mpango na maendeleo ya rasilimali watu;
Kuratibu ajira za wafanyakazi, uchaguzi, mafunzo ya mwelekeo, uwekwaji, kuthibitishwa, mafunzo na maendeleo ya waajiriwa, kupandishwa vyeo na uhamisho;
Kuandaa makadirio ya malipo ya mwaka ya mfanyakazi na kushughulikia na kuandaa mishahara;
Kuratibu utekelezaji wa mfumo wa PEPMIS
Kusimamia mafao ya mwajiriwa (pensheni, posho, kustaafu, kujiuzulu, kifo n.k) na stahili nyinginezo; kusimamia huduma zinazo husiana na huduma ya fomu ya kujitenga (kustaafu, kujiuzulu n.k);
Kuwezesha uhusiano wa mwajiriwa na ustawi ikiwa ni pamoja na afya ya mwajiriwa na usalama, michezo na utamaduni;
Kuchakata na kusasisha rekodi za likizo kama vile mapumziko, ugonjwa uzazi, masomo na mwisho;
Kuratibu madai na kushughulikia malalamiko;
Kuhudumu kama Sekretarieti kwa Kamati ya Uteuzi; na
Kuratibu Baraza la Wafanyakazi na masuala ya vyama vya wafanyakazi; na
Sehemu hii inaongozwa na Afisa anaye husika.
Sehemu ya Utawala
Sehemu hii inatekeleza shughuli zifuatazo:-
Kuwezesha ukarabati wa vifaa vya Ofisi, majengo na viwanja;
Kuratibu utekelezaji wa shughuli za kukuza maadiali, ambazo ni pamoja na kuzuia vitendo vya rushwa;
Kuratibu utekelezaji wa masuala mbalimbali;
Kutoa huduma za usajili, umesenja na utumaji na kusimamia kumbukumbu za Ofisi;
Kushughulikia masuala ya Itifaki;
Kuwezesha utoaji wa huduma za usalama, usafiri na huduma za jumla;
Kuratibu utekelezaji wa ushiriki wa Sekta Binafsi, uboreshaji wa mchakato wa biashara na Hati ya Huduma kwa Mteja katika Ofisi;
Kushauri kuhusu ufanisi wa Taasisi yo Ofisi;
Kuratibu shughuli za uchaguzi kwenye Halmashauri;
Kuratibu chaguzi kuu na chaguzi za Serikali za Mitaa; na
Kufuatilia utekelezaji wa kanuni za utawala bora.
Sehemu hii inaongozwa na Afisa anaye husika.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa