Tuesday 1st, July 2025
@Itongowa- Mngeta
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mlimba, Ndg. Jamary Idrisa Abdul amewapokea madaktari bingwa wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambao watakuwepo kwa juma zima wakitoa huduma bobezi za magonjwa ya wanawake na ukunga, magonjwa ya watoto na vichanga, na huduma za upasuaji na mfumo wa mkojo.
Nyingine ni huduma bobezi za magonjwa ya ndani, na huduma ya usingizi na ganzi. Muuguzi Mbobezi naye yupo sambamba na madaktari hao kuwahudumia wananchi wa Mlimba DC.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa