Pichani juu: kaimu mkurugenzi Wakili Faraja Nakua akimuonesha maeneo ya ujenzi Naibu Katibu mkuu wa Afya TAMISEMI Dr Doroth Gwajima (mwenye sketi Nyeusi na Skafu ya Tanzania)
Naibu katibu mkuu Afya TAMISEMI Dr. Doroth Gwajima ashauri uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba kubadili eneo la ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Halmashauri hiyo kutokana na mazingira yaliyopo kwa eneo lilichaguliwa.
Akizungumza mapema jana Dr. Gwajima alisema kuwa eneo lilichaguliwa lipo kwenye miinuko sana kitendo kitakachopelekea kuwatesa sana wauguzi pamoja na wagonjwa watakaokuja kutibiwa, kwani kuna wakati wagonjwa wataletwa wakiwa hawajiwezi sasa ikitokea watakaokuja hawana uwezo wa usafiri itawalazimu kupanda milima kitendo kitakachopelekea kushindwa kufanya hivyo.
Kutokana na hayo Dr. Gwajima aliwaamuru viongozi hao kukaa na kujadili mabadiliko hayo kabla ya kuyapeleka mkoani ambao na mkoa nao inabidi taarifa hiyo waifikishe kwake mapema sana kwaajili ya kuifanyia kazi.
Nae kaimu mkurugenzi wakili Faraja Nakua alisema kuwa wamelichukua wazo hilo na watalifanyia kazi mapema wiki hii na kupeleka taarifa mkoani kwaajili ya taratibu nyingine kama walivyoamriwa
‘’Tumepokea maagizo haya na tutakaa mapema wiki hii na kuyafanyia kazi maagizo yote uliyotupa mkuu na tutapeleka taarifa mkoani kabla ya wiki hii kuisha kwaajili ya utekelezaji.’’ Amesema wakili nakua.
Chini ni Habari picha
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa