Pichani juu: Kaimu Mkurugenzi, mwanasheria Faraja Nakua akipokea moja ya funguo za pikipiki ambazo zinatarajiwa kutumika katika mradi wa kunusuru zao la mpunga katika Halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
Meneja wa mradi wa kunusuru zao la mpunga Ifakara ndugu Marco Mbilinyi, mapema jana amemkabidhi Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero ndugu Faraja Nakua Pikipiki mbili kwaajili ya kuendeleza mradi huo kwenye Halmashauri hiyo.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi pikipiki hizo, Ndugu Mbilinyi amesema kuwa, utoaji wa pikipiki hizo ni mwendelezo wa mradi huo unaosimamiwa na Agakhan Foundation, wa kutoa vyombo vya usafiri kwa Halmashauri hii, kwani tayari imekwishatoa jumla ya Baiskeli mpya 12 kwa wakulima wakufunzi wanaosimamia na kuwafundisha wakulima wengine katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.
Awali Ndugu Mbilinyi alisema kuwa mradi huu unafadhiliwa na umoja wa ulaya na unatekelezwa katika wilaya tatu ambazo ni Malinyi, Ulanga na Kilombero, kwahiyo kwakuwa wanafanya kazi na serikali wameamua kuwa waangalizi wa mradi huu wawe maofisa wenyewe wa vituo, ambao watasimamia pia na shughuli nzima ya upokeaji wa posho kidogo za kila mwezi kwaajili ya mafuta na mambo mengine katika kufanikisha zoezi hilo.
Akipokea Pikipiki hizo, kaimu mkurugenzi mwanasheria Nakua amesema kuwa, kwa niaba ya mkurugenzi anatoa shukrani za dhati kupokelewa kwa vifaa hivyo, na kuahidi kuwa vifaa hivyo vitatumika katika kazi iliyotarajiwa kutumika na kamwe hazitafanya kazi nyingine, adidha alisema kuwa kwa kuwa Kilombero ndio injini ya kilimo cha mpunga, amewaomba kuiangalia kwa jicho la karibu na kuendelea kuisaidia kwa vifaa vingine vingi vya kilimo hususani cha mpunga, ili kuweza kuboresha kilimo hicho
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa