Mhe. Innocent Mwangasa Mwenyekiti wa Halmashauri ameongoza Mkutano wa Baraza la Kata la robo ya tatu kwa mwaka 2023/2024 na kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa kazi za kawaida za kata. Katika Mkutano huo, Waheshimiwa Madiwani wamemshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta mahitaji mbalimbali na kuwafariji wananchi wa kata ya Masagati na Utengule waliopata Mafuriko katika kipindi cha Mvua za Masika.
Waheshimiwa Madiwani wametoa Shukrani kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania @ikulu_mawasiliano , Mhe. Kassimu Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania @owm_tz, timu ya Mawaziri ikiongozwa na Mhe. Jenista Mhagama, Mhe. Godwin Kunambi @godwin_kunambi Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Mhe. Adam Kighoma Malima Mkuu wa Mkoa wa Morogoro @rs_morogoro , Mhe. Wakili Dunstan Kyobya @kyobyad @dc.kilombero na Viongozi pamoja na wananchi mbalimbali waliojitoa kuwasaidia wahanga wa Mafuriko katika Halmashauri.
Aidha, Waheshimiwa Madiwani wamemshukuru Ndugu Jamary I. Abdul @jamaryidrisa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kwa namna alivyoratibu maafa na kusaidia wananchi kupata mahitaji mbalimbali.
Pamoja na pongezi hizo, changamoto mbalimbali zimetolewa katika kata ikiwa ni pamoja na changamoto ya umaliziaji wa maboma ikiwa ni pamoja Hosteli katika Shule ya Sekondari Matundu Hill ambako boma limekamilika na kuhitaji Fedha za umaliziaji.
Katika hatua nyingine, pongezi zimetolewa kwa kata za Mchombe, Kamwene, Mbingu, Igima na Kata ya Namwawala kwa makusanyo ya mapato kwa kipindi cha Mwezi Machi 2024.
Maelekezo yametolewa kwa kata zilizofanya vibaya kwenye makusanyo kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa kudhibiti upotevu wa mapato ili kukamilisha miradi ya maendeleo kata ambazo hazikukusanya vizuri kata ya Mngeta, Utengule, Mofu, Idete na Masagati.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa