Pichani juu: Katibu tawala Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobero
KATIBU Tawala Wa Mkoa Wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo amesema kuwa Mkuu Wa idara yeyote ambae ushauri wake hauzingatii kanuni na Sheria na wenye lengo la kuiangamiza halmashauri basi mtu huyo hafai tena kuwa mkuu wa idara katika mkoa huo.
Mhandisi Kalobelo ameyasema hayo jana kata ya Mngeta wakati wa kikao cha Baraza Maalum la Madiwani Wa halmashauri ya Wilaya Mlimba la kujadili taarifa na majibu ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Akimwakilisha Mkuu Wa Mkoa huo,Mhandisi Kalobelo alisema ni jambo la kushangaza kwa Mtendaji kutoa ushauri katika vikao viiwe vya wakuu Wa idara ama baraza wakati akielewa ushauri huo anajua kabisa una lengo la kuiingiza halmashauri katika hasara.
Kauli hiyo ameitoa baada ya kuona moja ya hoja ambazo mdhibiti na mkaguzi Wa hesabu za serikali ameiona katika halmashauri hiyo ambayo inaonyesha halmashauri ilipata hasara ya shilingi milioni 430 kutoka kampuni ya Kilombero Plantatin Ltd (KPL).
Taarifa hiyo ibaonyesha kuwa halmashauri waliipatia KPL mashine ya kukatia ushuru kwa ajili ya zao LA mchele kwa kiwango anbacho kimahesabu kilizidi asilimia 3 ya bei ya soko kwa wakati huo na kwamba asilimia 3 ndio kiwango cha juu cha Sheria kwa tozo za ushuru Wa mazao.
Hata hivyo KPL ilishindwa kuilipa halmashauri na hatimae kupata hasara hiyo na katibu Tawala kuhoji ilikuwaje menejimenti iwakabidhi KPL Mashine ya kukusanyia ushuru badala ya zoezi hilo kulisinamia wenyewe.
Ameitaka menejiment kuhakikisha Fedha hizo zinarudishwa na Mtendaji yeyote atakaebainika anatoa ushauri kama huo atashushwa mamlaka kwani inaonyesha hana nia njema na halmashauri.
Katika hatua nyingine,Katibu tawala huyo ameitaka halmashauri hiyo kubuni miradi mingine mipya ili kuongeza mapato ya halnashauri ikiwemo zao za Michikichi ambalo linaonekana linastawi vizuri wilayani humo
Ameiagiza Tarura kuhakikisha barabara zinazoelekea katika uzalishaji zinarekebishwa ili kuweza kufikiwa kwa urahisi huku pia akiigiza idara ya Maendeleo ya Jamii kukusanya madeni ya wadaiwa Wa mikopo ya vikundi vya wanawake,Vijana na walemavu kabla ya Juni 30 mwaka huu.
Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji Wa halmashauri hiyo Mhandisi Stephano Kaliwa aliahidi kutatua changamoto zilizojitokeza huku akisema kuwa wametoa tani moja ya miche ya mikorosho kwa lengo la kuwa na zao mbadala ili kuongeza mapato ya halmashauri.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa