Jumanne Oktoba 21.10. 2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mlimba, Ndg. Jamary Idrisa Abdul alimpokea Kamishna wa Uchumi kutoka Tume ya Mipango Zanzibar akiwa na timu ya wataalamu kutoka wizara mbalimbali, taasisi za serikali na benki.


Timu hiyo ilijumuisha wataalam kutoka wizara ya kilimo, Taasisi ya Chakula na Dawa, Tume ya Mipango, Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar.

Akizungumza wakati wa mapokezi, Mkurugenzi Jamary amemshukuru Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuichagua Halmashauri ya Wilaya Mlimba kuwa sehemu ya fursa za kibiashara za zao la mpunga, akisema hatua hiyo inafungua milango ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya pande mbili.

“Kweli sisi tunaiona hii ni fursa kubwa. Itakuwa faida kwetu na kwa Zanzibar pia maana wao watachukua chakula na sisi tutapata fedha. Sisi tutatoa ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha fursa hii inatekelezwa”, alisema Mkurugenzi Jamary.
Kwa upande wake Kamishna wa Uchumi kutoka Tume ya Mipango Zanzibar, Dkt. Ameir Sheha amesema ziara hiyo inalenga kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kuhusu kuhakikisha Zanzibar inapata bidhaa za chakula kwa bei nafuu kutoka Tanzania Bara, ikiwemo mpunga kutoka halmashauri za mlimba, Ifakara na Malinyi.
Dkt. Sheha ameongeza kuwa timu yao baada ya kutembelea halmashauri hizo, itakutana na taasisi za mkoa, zinazo shughulika na uendelezaji wa zao hilo ili kuona namna bora ya kuimarisha biashara hiyo kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.
Amehitimisha kwa kushukuru mapokezi mazuri waliyoyapata kutoka kwa viongozi na wananchi wa mkoa wa Morogoro, akisema hatua hiyo inaonesha utayari wa pamoja katika kuimarisha biashara kati ya Zanzibar na Bara.
“Tangu tumeingia Morogoro naona tumekuwa katika mikono salama kuanzia kwa Afisa TAwala Mkoa, DC pale Ifakara, lakini tumekuja hapa Mlimba, Fantastic. Kweli inaonesha watu wako tayari kwa hii kazi. Mimi niseme tunashukuru sana.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa