Pichani juu: Mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi akionyesha samaki ambao hawakustahili kuvuliwa kwa afisa habari wa halmashauri ya wilaya ya kilombero.
katika hali isiyokuwa ya kawaida mchuuzi wa samaki bwana Denis ferdinand amekamatwa akiwa na samaki wadogo huku akiwa hana leseni katika eneo la Namwawala tayari kwa kuwasafirisha kwenda kuwauza mapema jana.
akizungumzia sakata hilo, mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi bi Annete Kitambi alisema kuwa mchuuzi na mvuvi huyo alikamatwa akiwa katika harakati za kuwavusha samaki hao kimagendo, huku akijua wazi kuwa kufanya hivyo ni kunyume na utaratibu unavyotakiwa kuwa.
akijibu tuhuma hizo ndg Ferdinand alisema kuwa ni kweli kuwa anakiri kosa na yupo tayari kulipa faini ingawa alisema kuwa huwa anatumia leseni yake aliyokutwa nayo ambayo siyo kwaajili ya Halmashauri ya wilaya ya kilombero bali aliikatia kwenye mamlaka ya Ifakara mji. na kuhusu suala la kuwa na samaki wadogo sana ambao kwa mujibu wa sheria na wanavyotakiwa kuwa haikutakiwa kabisa kuvuliwa, alisema kuwa hakujua kuwa hilo ni kosa hivyo aliomba msamaha kwa kosa hilo.
Akijibu swali la kuwa samaki hao wanatakiwa kuwa na ukubwa gani ndipo wavuliwe, Bi Kitambi alisema kuwa samaki hao kwa kawaida huwa na kilo kuanzia ishirini mpaka thelathini hivyo kuwahi kuwavua wakiwa wadogo kiasi hicho ni kupoteza mali asili yetu na fahari yetu kwani watakapovuliwa wadogo kiasi hicho itachangia kwa kiasi kikubwa kumaliza kizazi hicho na hivyo kuangamiza zalio (species) hilo.
Aidha Bi kitambi alimuamuru kulipa faini ambayo ni kiasi cha shilingi laki moja na kuamuriwa samaki hao kupigwa tena mnada ambapo pia aliamua kuwanunua yeye mwenyewe ili kuepusha hasara kubwa ambayo angeweza kuipata.
''kwa mujibu wa sheria ni kosa kubwa sana kufanya biashara ya kuvua ama kuchuuza samaki bila ya kuwa na leseni ya kufanya hivyo kutoka kwa halmashauri ya kilombero ikiwa tu biashara hiyo utaifanya kwenye mamlaka ya kilombero, hivyo pamoja na yote hayo unatakiwa pia kukata leseni mara moja ili uweze kufanya kazi yako kihalali''. Alimaliza bi Kitambi.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa