Mkuu Wa mkoa Wa Morogoro Dk Steven Kebwe amekerwa na idadi kubwa ya wanafunzi Wa sekondari wilayani Kilombero kukatishwa masomo yao baada ya kupewa mimba huku akitoa onyo kwa Hakimu yeyote anaecheza na kesi za mimba kwa wanafunzi atakula nae Sahani moja.
Kauli hiyo ameitoa jana mjini Ifakara baada ya kufanya kikao cha pamoja baina yake na wakuu Wa shule na waratibu elimu kata Wa Wilaya ya Kilombero katika shule ya sekondari Ifakara chenye lengo la kupata taarifa za usimamizi Wa elimu katika Wilaya hiyo.
Katika taarifa za hali ya elimu katika halmashauri Mbili za Kilombero na Mji Ifakara ilionyesha kuwa wanafunzi 63 Wa sekondari walipata mimba hivyo kuacha masomo yao kwa mwaka 2017.
Dk Kebwe alisema idadi hiyo ni kubwa hivyo amemuagiza Mkuu Wa Wilaya kuhakikisha kwamba wale wote waliohusika na kuwapa wanafunzi hao ujauzito wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria haraka iwezekanavyo.
Mkuu huyo Wa mkoa pia ametoa onyo kwa Hakimu yeyote atakaecheza na kesi ya mimba kwa mwanafunzi atamshughulikia sababu wapo baadhi yao wanacheza na wazazi Wa watoto ama wahusika na kupindisha Ukweli ama kuchelewesha ushahidi.
Amezitaka Mahakama kuharakisha kesi zote zinazohusu ujauzito kwa wanafunzi na mahakimu wasilete kisingizio cha ushahidi wakati inaonyesha kabisa wanafunzi hao walirubuniwa kwa umri wao Mdogo ama tamaa na wahusika wapo humohumo mitaani.
Kuhusu utekelezaji Wa agizo LA Rais MAgufuli LA kutaka wazazi kutochangia michango mashuleni,Mkuu huyo Wa mkoa alisema kama mkoa ameunda kamati maalum ya kufuatilia walimu wanaochangisha wazazi na kubainisha kuwa Kamati hiyo itajumuisha watu watano kutoka mkoani na pia Wilaya zote na ameipa siku 14 kumpelekea taarifa mezani kwake.
Alisema walimu wakuu na wakuu wa shule wahakikishe wanafuata utaratibu kama ambavyo unafafanuliwa vizuri katika waraka Wa sita Wa mwaka 2016 na wazazi ama walezi wasipewe mzigo Wa michango na pale amvapo wanakubaliana kwa Uhuru wao bila shinikizo ruksa kuchangia lakini bila shuruti.
Kwa mujibu Wa Mkuu huyo Wa mkoa kuwa kila mwezi kwa sasa mkoa unapewa kiasi cha shilingi bilioni 1.3 toka serikali kuu kwa ajili ya kutekeleza Sera ya elimu bila malipo na kusema kuwa atashangaa walimu ama kamati za shule zikiendelea kunga'ang'ania kuwachangisha wazazi wakati Fedha zinafika mashuleni kwa wakati ili kutekeleza Sera hiyo.
Kwa upande wake Afisa elimu mkoa Wa morogoro Euphransia Bubhuma alisema kwa mwaka 2017 hali ya ufaulu ilipanda toka nafasi ya 27 mwaja 2016 hadi nafasi ya 11 kitaifa mwaka jana kwa matokeo ya darasa LA saba na darasa LA nne walitoka nafasi ya 15 mwaka juzi hadi nafasi ya 11 mwaka jana.
Bubhuma alitaja mkakati Wa mkoa katika kuinua kiwango cha taaluma ni pamoja na kusimamia mahudhurio ya wanafunzi darasani sambamba na kusimamia ufundishaji Wa dhati kwa walimu darasani na utoaji Wa chakula kwa wanafunzi ili kuwajengea uwezo darasani.
Kuhusu changamoto za mimba mashuleni alisema warahakikisha wale wote watakaohusika wachukuliwe hatua za kisheria na walimu watoe elimu ya kijinsia kwa wanafunzi Wa kike ili kumaliza tatizo hili.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa