Wenyeviti wa Vyama vya Ushirika vilivyomo kwenye Halmashauri ya Mlimba, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha UKICU, wamefanya kikao kutathmini mwenendo wa mauzo ya mazao ya Kakao na Ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ambao Halmashauri ya Wilaya Mlimba imeanza kuutumia mnamo mwezi Juni, 2024.
Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Mlimba ndg. Juma Abeleu amesema tangu Juni 12, 2024 Halmashauri ilipoingia kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani mpaka sasa, jumla ya minada minne ya Kakao imefanyika, kilo 117,180 za Kakao zimeuzwa na kuwaingizia wakulima jumla ya shilingi 2, 205,928,200 huku Halmashauri ikiwa imepata ushuru shilingi 80,317,314 ambayo ni asilimia tatu ya mauzo ya zao husika.
Kando ya mafanikio hayo, wanakamati walitaja changamoto zinazo kabili zoezi la uuzaji wa mazao kwa njia ya stakabdhi ghalani. Miongoni mwa changamoto hizo ni baadhi ya wakulima kutoridhika na bei na kutaka kutoa mzigo yao ghalani, uhaba wa wataalamu kwenye baadhi ya vyama vya msingi, upinzani kutoka kwa wafanya biashara na madalali wa mazao.
Nyingine ni watu kutojua jinsi mfumo wa stakabadhi ghalani unavyofanya kazi na faida zake kwa wakulima, ugumu wa usafirishaji wa mazao kutoka AMCOS kwenda ghalani, ucheleweshwaji wa malipo toka AMCOS kwenda kwa wakulima, uhaba wa vifungashio na ukosefu wa benki ya Kokoa mbichi.
Hata hivyo, wana kamati hawakuishia kutaja changamoto tu bali wametoa maoni yao ya nini kifanyike kuondoakana nazo, ikiwemo kuhakikisha elimu kuhusu mfumo wa stakabadhi ghalani, manufaa ya mazao ya kimkakati, ubora wa bidhaa inapelekwa moja kwa moja kwa wakulima, kuwepo na vifungashio vyenye nembo ya Chama Kikuu cha Ushirika cha UKICU na Watendaji wa Kata na Vijiji kujengewa uwezo kuhusu zoezi zima la uuzaji wa mazao kupitia stakabadhi ghalani ili waweze kuongeza nguvu katika kuelimisha wakulima kuhusu mfumo huo.
Naye Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha UKICU amewataka wenyeviti wa AMCOS kutambua kwamba sasa wanapaswa kuimarika katika vyma vyao ili walanguzi wasiwe na nguvu kuliko Vyama vya Ushirika ama wakulima.
Amesema hiyo itasaidia pindi mkulima anapokubali bei pasiwepo na kigugumizi katika kuendelea na bei hiyo, kama ambavyo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kutokana na kwamba kwa sasa madalali na wafanyabiashara ambao wengi wao hawana nia njema na mnada, ndio wanaoleta mazao ghalani na sio mkulima.
Amewataka wenyeviti hao wawapo ghalani wakati wa mnada wazingatie zaidi wakulima na sio nani kaleta mazao ghalani.
MWISHO
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa