Pichani juu: Naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Mhe. Musa Sima (aliyesimama) akizungumza na viongozi wa wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi.
Viongozi katika Bonde la Kilombero wamehimizwa wawe na ushirikiano katika utendaji Wa kazi zao ili kulinusuru Bonde hilo.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Wa nchi,Ofisi ya Makamu Wa Rais Muungano na Mazingira Musa Sima wakati akizungumza na viongozi Wa Wilaya za Kilombero,Ulanga na Malinyi katika mkutano uliofanyika mjini Ifakara.
Sima amesema kama watendaji na viongozi Wa kuchaguliwa wakifanya kazi kwa pamoja na baadae kutoa elimu kwa wananchi ana imani hakutakuwa na migogoro katika Bonde hilo ambalo ndio tegemeo la Maji katika mto Rufiji.
Amesema kama kila kiongozi akifanya kazi kwa matakwa yake basi migogoro na uharibifu wa bonde hilo utaendelea kuwepo sababu hakutakuwa na kiunganishi baina ya wananchi na serikali.
Naibu waziri aliyasema hayo baada ya awali kuwasikiliza wakuu Wa Wilaya hizo na wenyeviti Wa halmashauri kuelezea hali halisi ya Bonde la Kilombero ambapo kila upande ulimlaumu mwenzake kuwa kwa namna moja ama nyingine unachangia uharibifu huo.
Wakuu Wa Wilaya walisema kuwa juhudi kubwa zinafanywa kwa ushirikiano Wa wakuu Wa Wilaya zote tatu ila inapofikia katika utekelezaji Wa maagizo wanasiasa uwakingia kifua wananchi na hali hiyo usababisha mambo kuharibika.
Kwa upande wao wenyeviti Wa halmashauri walisema kuwa tatizo lipo kwa baadhi ya watendaji ambao utoa maagizo ya ghafla kwa wananchi bila kuwaandaa na kudai kuwa hakuna anaepinga uhifadhi Wa Bonde hilo ila taarifa zinatakiwa kutolewa kwa wakati.
Naibu waziri alisema inaonyesha kuwa hakuna ushirikiano Wa karibu katika kulilinda Bonde hilo hivyo kuwataka viongozi kuwa na ushirikiano Wa pamoja kabla na baada ya kufanya maamuzi kisha kuwapa elimu wananchi na hiyo haitasababisha migongano.
Ametolea mfano kuwa Rais Magufuli anaaminiwa na wananchi wote Wa chini kwa sababu anawasikia hivyo kwa nini viongozi Wa chini hawaaminiwi na wananchi?,alihoji.
Kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa kijiji cha Ngombo baada ya mawaziri 8 kutembelea eneo hilo hivi karibuni ,Sima aliwataka viongozi wa Wilaya hizo wawe na subira kwani hivi karibuni watampatia maelekezo na ushauri Rais na yeye kutoa majibu.
Alisema toka walipofika katika kijiji hicho na maeneo mengine timu ya mawaziri 8 wamegundua mapungufu kadhaa ikiwemo maeneo mengine kuwa chepechepe huku maeneo mengine yakionekana vitongoji ndio vimeingia katika hifadhi na sio kijiji kizima
Hata hivyo naibu waziri huyo amewataka watendaji wawe na utu na sio kung'ang'ania tu Sheria wanapotaka kuwatoa wananchi kwani iwananchi wanapenda hifadhi ila binadamu nao wana thamani yao.
Ametoa maagizo kwa wataalamu Wa mazingira kupeleka kwa wakuu Wa Wilaya mpango kazi Wa uhifadhi Wa ikolojia na uhifadhi Wa mazingira na kuwepo na kamati za mazingira kuanzia ngazi ya chini na ziwe kamati hai.
Awali wakuu Wa Wilaya hizo walimweleza naibu waziri kuwa wana ushirikiano Wa pamoja katika kulitunza bonde la Kilombero na sasa wanasuburi kauli ya serikali kuhusu kijiji cha Ngombo kutokana na hivi sasa kuwepo na mapigano baina ya wakulima na Wafugaji kugombea kijiji hicho.
Kwa upande wao wakurugenzi na wenyeviti Wa halmashauri na mhifadhi pori tengefu la Kilombero walisema changamoto kubwa inayolikabili Bonde hilo kwa sasa ni uvamizi Mkubwa Wa mifugo .
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa