Afisa Elimu Msingi na Awali Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Bi. Witness Kimoleta amefanya kikao na walimu wa Shule za Msingi, Igima, Matalawani, Mbingu, Matete na Londo ambazo zipo katika ya Igima na Mbingu. Afisa Elimu katika kikao hiko amesisitiza zaidi walimu kuweza kutambua wajibu na majukumu yako ya kikazi, ujazaji wa taarifa katika Mifumo ya Kiutumishi, kuhamasisha Wazazi kufahamu umuhimu wa lishe Mashuleni pamoja na wazazi kuwaandikisha watoto shuleni hasa wenye umri wa kuanza shule za awali na Msingi kwa Mwaka 2024.
Aidha, Afisa Elimu Amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Samia Suluhu kwa kuleta fedha za utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi ambapo imesaidia wanafunzi kutotembea umbali mrefu kupata huduma ya Elimu, kupunguza msongamano wa wanafunzi wengi darasani na kutoa Elimu katika Miundombinu iliyo bora na salama.
Pia Shule ya Msingi Igima ni shule Mpya iliyojengwa kwa Fedha za Utekelezaji wa Mradi wa Boost ambayo ina thamani ya kiasi cha Shilingi Milioni Mianne Sabini na tano na laki tatu iliyongea Vyumba kumi na nne vya madarasa ya Elimu Msingi, Madarasa mawili ya Awali, na Jengo Moja la Utawala
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa