Afisa elimu msingi wa Halmashauri ya wilaya ya kilombero Bi.Witness Kimoleta amewagiza maafisa Elimu kata na wakuu wa shule za msingi zote katika wilaya ya Kilombero kuwa majengo mazuri shuleni kutumiwa na wanafunzi wa darasa la kwanza hadi darasa la tatu ili kuwatengeneza msingi bora wa taaluma kwa wanafunzi hao
Hayo amesema katika kikao cha tathimini na mikakati ya ufundishaji kwa mwaka 2019 ,tarehe 3/1/2019 na Maafisa elimu kata na wakuu wa shule za msingi wilaya ya Kilombero katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, amesema mazingira mazuri humsaidi mtoto kufaulu mitihani ya kujipima kwa darasa la nne na kufaulu darasa la saba.
" Darasa la kwanza hadi darasa la tatu yameonekana kama ni madarasa ya dharura,sasa kupitia kikao hiki natoa maagizo kwamba madarasa yote mazuri shuleni yawe ya wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu ili kuwajengea msingi mzuri"amesema Kimoleta
Akizungumzia matokeo ya ufaulu kwa mwaka 2017/2018 amesema idadi ya watahimiwa na ufaulu umepanda jambo ambalo linatoa mwanga kwa ubora wa utendaji kazi na kuwataka waongeze juhudi katika ufundishaji bila kutazama changamoto zilizopo huku akiwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuifanya wilaya ya Kilombero kushika nafasi ya nne kimkoa na nafasi ya 54 kitaifa katka matikeo ya mwaka jana.
Katika hatua nyingine aliwataka walimu na maafasa kata kuwa wabunifu kwa kushirikisha na wadau na kamati mbalimbali katika kutatua changamoto zinazo wakabili wakati wa kutekeleza majukumu yao huku akizitaja baadhi ya changamoto hizo ni upungufu wa walimu,miundimbinu na ongezeko la watoto wanaoandikishwa mashuleni na kuwaomba kuwa na uvumilivu na lengo moja la kufanyakazi kwa bidii.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa