Mkurugenzi Mtendaji Eng. Stephano B. Kaliwa akiwa pamoja na wakuu wa Idara na watendaji kata wakisikiliza Tathimini ya Lishe kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022.
Halmashauri ya Mlimba imefanya tathimini ya shughuli za Lishe katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2021/2022 katika vijiji vyote 62, kata 16, vituo vya kutolea huduma za afya 43.Pia idara Mtambuka za Lishe ambazo ni kilimo,Elimu Msingi, Elimu Sekondari na Maendeleao ya Jamii nazo zimekuwa zikitekeleza shughuli za Lishe
Ndugu, Bodygadi S. Buhari Afisa Lishe (W) amesema, Halmashauri ilitenga kutumia mapato ya ndani takribani 60,930,550 na mpaka mwisho wa mwaka wa fedha june, 2022 takribani 58,761,233.6 zimetumika ikiwa ni 96.44%
Baadhi ya shughuli ambazo zimekuwa zikitekelezwa katika kupambana na utapiamlo miongoni mwa watoto chini ya miaka mitano, akina mama wajawazito, wanaonyonyesha na watu wazima ni pamoja na kutoa elimu ya Lishe kwa jamii, kutoa matibabu ya utapiamlo mkali, kufanya ukaguzi wa usalama na ubora wa vyakula, kuwa na kamati imara ya Lishe ngazi ya Halmashauri na kuendesha vikao kila robo mwaka, kufanya maadhimisho ya siku ya afya na Lishe kila kijiji kwa kila robo mwaka, kuadhimisha wiki ya unyonyeshaji, kuendesha kampeni ya mwezi wa afya na Lishe (CHNM), Upimaji wa madini joto kwenye chumvi, kufanya ukaguzi wa vyakula, kutoa vidonge vya kuongeza wingi wa damu kwa akina mama wajawazito, kufanya utambuzi wa hali ya Lishe kwa makundi mbalimbali.
Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuwa na wodi maalumu ya kuwatibu watoto wenye utapiamlo mkali, kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya Jamii 105 kwa ajili ya kutekeleza shughuli za Lishe kwenye jamii, kuchapisha nakala za vitabu kwa ajili ya kutolea taarifa za Lishe kwenye kata zote na vijiji vyote, kuimarisha utoaji wa elimu ya Lishe katika vituo vya kutolea huduma za afya, kuendesha vikao vya tathmini ya Lishe vikishirikisha watendaji wa kata ambao wanawakilisha jamii.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa