Pichani juu : Aliyekuwa afisa Kilimo ndg. Mohammedi Ramadhani, akizungumza na watendaji wenzake wa Kilombero.
Aliyekuwa afisa kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero ndg Mohammedi Ramadhani mapema leo alitumia nafasi aliyopewa na mkurugenzi mpya wa Halmashauri hiyo Eng. Stephano Kaliwa kuwaaga watendaji wenzake na kuelekea kwenye Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi akiwa kama mkurugenzi mpya wa Halmashauri hiyo.
Akizungumza kwa majonzi makubwa, ndg Ramadhani amesema kuwa, kuteuliwa kwake kumetokana na ushirikiano mkubwa sana uliopo, baina ya wafanyakazi waliokuwa wakishirikiana nae, hivyo anaondoka huku akiwa anajua kabisa kuwa, anakokwenda ni nyumbani ingawa na alipotoka ni nyumbani pia.
Aidha, ndg Ramadhani alitumia nafasi hiyo, kuwaomba wafanyakazi wa Kilombero kuendeleza ushirikiano baina yao kwani bila hivyo, hakutkuwa na maendeleo yatakayopelekea kufikia malengo waliyojiwekea.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa