Naibu waziri ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi) Mh. Seleman Jaffo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero pamoja na watumishi wa Halmashauri ya mji wa Ifakara katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya Kilombero mjini Ifakara.
Mh. Jaffo amesema Barabara ya Kidatu - Ifakara ujenzi wake uko mbioni kuanza wakati wowote kutoka hivi sasa kwa kiwango cha Rami kwa ufadhili wa umoja wa jumuiya za nchi za ulaya (european union) teyali fedha zimeshapatikana na mkataba umeshasainiwa na katibu mkuu kutoka wizara ya fedha ikiwa ni kazi kubwa iliyofanywa na Mh. rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.
Aidha naibu waziri amefafanua kuwa lengo ni kuwafanya watumishi pamoja na wananchi kwa ujumla kufanya kazi zao kwa amani ikiwa ni pamoja na kurahisisha usafirishaji wa mazao ya wakulima kwa urahisi zaidi baada ya kukamilika kwa barabara.
Ziara ya Mh naibu waziri ilikuwa na lengo la kukagua miradi ya maendeleo na kuongea na watumishi ikiwa ni sehemu ya kufahamiana na kupeana maelekezo ya kazi kwa watumishi wa serikali za mitaa.
Katika khotuba yake naibu waziri amewaeleza watumishi wa Kilombero kuwa dhana ya mabadiliko lazima watendaji wa serikali wabadilike katika utendaji wao wa kazi ambapo amewataka watumishi katika halmashauri zote mbili kila mtumishi ni lazima atimilize wajibu wake ili kuwatumikia wananchi.
Wakati huohuo Mh. jaffo amewasisitiza watumishi hususan wakuu wa idara kupangiana malengo kwa kujaza fomu za upimaji malengo ya kazi kwa mwaka wa fedha 2017/2018 huku akihitaji kupata nakala ya fomu za wakuu wa idara wa nne kutoka idara ya maji , afya, kilimo na idara ya ujenzi ili aweze kuona malengo waliyokubalina kuyafanya kwa mwaka wa fedha 2017/2018 pia Mh. naibu waziri amehitaji nakala ya watendaji kata wanne ambao wameshafanyiwa upimaji wa tathmini zao kutoka katika kata.
Akihitimisha khotuba yake Mh. Jaffo amemtaka mkuu wa idara ya maji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero kumpatia taarifa ya miradi ya maji inayotekelezwa ndani ya halmashauri ya wilaya ya Kilombero pamoja na changamoto zinazoikabili miradi hiyo ifikapo jumatano ya tarehe 09/08/2017 ikiwa inaonyesha kama wakandarasi wako katika eneo la kazi ama hawako na lini miradi hiyo itakamilika. Mh waziri pia amewapongeza watumishi wa wilaya ya Kilombero kwa kufanya kazi kwa ushirikiano kati ya wakuu wa idara, watumishi, mkurugenzi pamoja na mkuu wa wilaya huku akilinganisha tofauti aliyoiona katika maeneo mengine aliyoyatembelea ndani ya halmashauri zilizopo mkoani Morogoro.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa