pichani juu: Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya kilombero, Eng. Stephano Kaliwa, akimkabidhi Diwani wa kata ya Namawala, ndg Muya Jovin Msulwa, kanuni za kutendea kazi madiwani
Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya kilombero, jana limeendelea na vikao vyake vya kisheria kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Halmashauri, katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero.
Katika kukamilisha suala zima la utekelezaji wa vikao hivyo, halmashauri imeendelea kujadili kuhusu mambo mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo miradi kama ya elimu, maji, na mengineyo.
Aidha baraza limetumia fursa hiyo kuweza kumuapisha diwani mpya wa Namawala mheshimiwa Muya Jovin Msulwa, Ambae baada ya kiapo hicho aliendelea na vikao vya baraza akiwa kama diwani kamili.
Katika hatua nyingine mkurugenzi alimkabidhi kanuni na makabrasha yatakayomuongoza katika utendaji kazi wake, akiwa kama diwani atakaeweza kuudhuria kwenye vikao vyote.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa