Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Kilombero katika kikao chake cha robo ya tatu kilichofanyika tarehe 27.04.2017 kimewataka wataalam wa skimu za umwagiliaji kutoka kanda ya mashariki kutatua changamoto za skimu za umwagiliaji katika miradi ya sululu na mbingu kwa kuzifuatilia kwa ukaribu na kutoa majibu yanayoridhisha.
Mwenyekiti wa kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira Mh John Chelele ambaye ni diwani wa kata ya Chita alikiambia kikao kuwa wataalam wa kanda wanaosimamia miradi ya skimu za umwagiliaji walifika katika kikao cha kamati na kutoa maelezo ya miradi hiyo ya umwagiliaji ambayo hayakuwaridhisha wajumbe wa kamati, kutokana na wataalam hao kuonekana kutokuwa na ufahamu wa uhalisia wa hali ilivyo katika miradi hiyo ya umwagiliaji.
Wakichangia kwa pamoja Mh. Hilda Mahimbali diwani wa viti maalum tarafa ya Kidatu na Mh. Erasto Mwanyika diwani wa Ching'anda walisisitiza kuwa wataalam hao walielekezwa kwenda kujipanga upya na kuja na ripoti inayojitosheleza kuhusu miradi hiyo ya umwagiliaji hususan katika miradi ya sululu na miradi ya mbingu.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa