Pichani juu: Naibu waziri wa TAMISEMI Mhe. Josephat Kadenge akikagua bidhaa zinatengenezwa na kikundi cha wakina mama wanaoishi na virusi vya Ukimwi cha upendo.
BARAZA la wanaoishi na virusi vya Ukimwi katika Wilaya ya Kilombero (KONGA) kwa kushirikiana na taasisi ya SAUTI Yetu wametenga kiasi cha shilingi milioni 20.8 ili kutekeleza shughuli za watu wanaoishi na virudi vya ukimwi katika kata tano katika halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Akitoa taarifa mbele ya kamati ya kudumu ya bunge ya mambo ya ukimwi,Mwenyekiti Wa KONGA Halida Kumba amesema Fedha hizo wametenga katika mwaka Wa Fedha 2018/2019 na kata zitakazonufaika ni Kidatu,Mang'ula B,Chita,Mlimba na Utengule.
Kumba amesema kupitia baraza lao halmashauri zote mbili pia zimeweza kuvipa vikundi 18 mtaji Wa kuanzisha shughuli za ujasiliamali na kutoa elimu jinsi ya kuendesha shughulu zao za kiuchumi.
Kuhusu vikundi,amesema halmashauri ya Wilaya ya Kilombero wamefanikiwa kuanzisha vikundi 40 vyenye wanachama 486 na halmashauri ya mji wa Ifakara ina vikundi 10 vyenye wanachama 107 na bado wanaendelea kuhamasisha wanaoishi na virusi kujiunga katika vikundi.
Aidha Kumba ameipongeza serikali kwa kuwanufaisha waathirika kwa kuwapatia dawa kwa wakati na wamekuwa wafuasi wazuri Wa tiba na wamefubaza VVU mwilini na pia wameweza kuwafikia makundi maalum kama vile watoto na Vijana balehe.
Hata hivyo,Mwenyekiti huyo ametaja changamoto wanazokumbana nazo ikiwemo umbali wa vituo vya kutolea huduma, hivyo kusababisha kuongeza ufuasi mbaya Wa dawa na utoro vituoni na wanaoishi na virusi kukosa mitaji kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi, hivyo kuiomba serikali kuu iongeze ruzuku kwa halmashauri ili vikundi vya waathirika viweze kufikiwa.
Kwa upande wake Mratibu Wa ukimwi katika halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Hawa Mdoka alisema kama halmashauri, wapo sambamba na KONGA na wametoa kadi 305 za mfuko Wa Afya CHF kwa wanaoishi na virusi vya ukimwi, katika halmashauri hiyo.
Naye Mwenyekiti Wa kamati ya kudumu ya ukimwi Oscar Mukasa, amesema, watahakikisha wanawasiliana na serikali ili kusaidia baraza hilo, kutokana na umuhimu uliopo na kuzitaka halmashauri hizo ziwatazame kwa umakini taasisi zote zinazojishughulisha na uangalizi wa wanaoishi na virusi vya Ukimwi, hasa vikundi vya wanawake ikiwemo kikundi cha Upendo cha Ifakara.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa