pchani mtoto Grace Songolo mara baada ya kufikishwa katika hospitali ya K1 Kidatu.
Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya nyandeo, mtoto Grace Songolo, pichani akigugumia maumivu baada ya kuvunjika mguu alipokuwa akishiriki michezo ya UMISETA kwa ngazi ya kata kwa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, siku ya ijumaa iliyopita ya tarehe 20/4/2018
kwa sasa mwanafunzi huyo ameruhusiwa kwenda nyumbani kwa uangalizi zaidi baada ya hospitali ya K1 Kidatu kumhudumia na kuweza kufanikiwa kumrudisha katika hali yake ya kawaida huku maumivu yakiwa yamepungua kabisa.
Awali mipango ilikuwa inafanyika kwenye ofisi ya afisa elimu wa halmashauri ya wilaya ya kilombero ili kuhakikisha kuwa wanamsafirisha mtoto huyo kumpeleka hospitali ya tiba maalum ya mifupa Tumbi kwaajili ya matibabu zaidi kabla ya hospitali ya K1 Kidatu kutoa maelezo ya kufanikiwa kumpa tiba ya uhakika mtoto huyo. Hadi tovuti hii inakwenda mitamboni, haikubahatika kuongea na mtoto huyo kujua ni kitu gani hasa kilichosababisha mpaka kuteleza na kuumia, kutokana na ukweli kwamba alihitaji muda wa kutosha kuweza kupumzika
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa