Pichani juu: Mkuu wa wilaya ya Kilombero Chief James Ihunyo akitoa zawadi za pesa taslimu kwa baadhi ya wananchi waliozidisha Hamasa katika mradi wa mabweni ya shule ya Upili ya Sanje
Mkuu wa wilaya ya Kilombero Chifu James Ihunyo, amesema kuwa amefurahishwa na watu waliojitoa kwa mioyo yao yote, katika kusherehesha shughuri ya Mwenge wa Uhuru, kwa lengo la kufanya muonekano mzima wa wa shughuli hiyo ifane na kupendeza.
Aidha ili kuidhihirisha furaha yake Mkuu wa Wilaya hiyo, aliamua kutoa zawadi za pesa taslim kwa baadhi ya wananchi ambao, walionekana kunogesha shughuli zaidi, kwani kwa kufanya hivyo kulipelekea kuamsha baadhi ya watu waliokaa kimya kuungana na washereheshaji wengine kwa lengo la kuchangamsha shughuli hiyo.
Katika mazungumzo yake, Chifu Ihunyo alisema kuwa kilichopelekea yeye kutoa pesa nyingi kwa wananchi katika kusherehekea mwenge wa uhuru uliopita katika Halmashauri ya wilaya ya Kilombero tarehe 05/08/2019, ni kutokana na watu kuhamasishwa vya kutosha na kupelekea shughuli hiyo kuwa ya kipekee miongoni mwa Halmashauri zote katika mkoa wa Morogoro.
Awali ilionekana kuwa mkuu huyo wa wilaya alikuwa akishiriki kucheza na wananchi waliojitokeza na kutoa shamra shamra huku akitoa zawadi mbali mbali zikiwamo pesa taslim kwa wananchi waliojijitokeza kitendo kilichopelekea wananchi hao kujitokeza kwa wingi hata kwenye mashindano kadhaa yaliyoandaliwa na mkuu huyo.
Katika Hatua nyingine Mkimbiza mwenge wa kitaifa ndugu Mzee Mkongea Ally, akiwaaga wananchi waliojitokeza katika mkesha huo katika eneo la kiberege katika halmashauri ya wilaya ya Kilombero, amesifu namna hamasa ilivyofanyika na kupelekea watu kubaki wengi kwenye mkesha ambapo watu hao wangeweza kulala majumbani kwao lakini kwa uzalendo tu wa taifa lao na mwenge kwa ujumla, wameweza kukesha na mwenge.
''Niwashukuru sana wananchi ambao mmeacha usingizi wenu na kuja kusherehekea na sisi kwenye mkesha huu wa mwenge kwa mwaka huu, kwa kweli tumefarijika sana, kwani hamasa iliyofanyika ni kubwa sana, najua mngeweza kulala majumbani mwenu lakini mmeonesha ushirikiano na uzalendo mkubwa sana mungu awabariki sana na kwaherini.'' Alimaliza.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa