MKUU Wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo sambamba na kamati yake ya ulinzi na Usalama wakishirikiana Mamlaka ya Usimamizi Wa Wanyamapori(TAWA)wamefanya zoezi la kushtukiza na kukamata ng'ombe zaidi ya 100 waliovamia hifadhi na maeneo ya wakulima.
Zoezi hilo la aina yake lilifanyika Jana katika kata ya Mofu na Dc huyo hakutaka kuwajulisha mapema viongozi Wa kata hiyo kwa kuhofia kuvujisha siri kwa wafugaji hatimae kutorosha Mifugo yao.
Baada ya kuingia Mofu yaligawanya makundi matatu tayari kusaka Mifugo iliyoingia kinyemela na ile inayolishwa katika Mashamba ya wakulima na hatimae kundi lililoongozwa na Mkuu huyo Wa Wilaya lilifanikiwa kukamata ng'ombe zaidi ya 50.
Hata hivyo zoezi hilo halikufanikiwa kukamata ng'ombe wengi tokana na kuchelewa kufika katika kata hiyo na hiyo ilipelekea baada ya kuonekana tu wafugaji walianza kuwasiliana kwa simu na hatimae makundi makubwa ya ng'ombe kukimbizwa ama kufichwa msituni.
Ihunyo amesema ameamua kufanya zoezi la kushtukiza baada ya kupewa taarifa na raia wema kuwa hivi sasa katika kata hiyo ya Mofu kuna Mifugo mingi imeingia kutoka Wilaya Jirani ya Malinyi na kwa sasa wanachungia katika Mashamba ya wakulima na kufanya wakulima hao kushindwa kulima mahindi baada ya kivuna mpunga.
Mkuu huyo Wa Wilaya alisema toka mwaka 2012 katika kata nzima walitenga maeneo ya wakulima na wafugaji lakini anashangaa bado baadhi ya wafugaji wabishi na wanaendelea kuingiza Mifugo na kulishia katika Mashamba ya wakulima na hiyo inahatarisha kuleta migogoro ya wakulima na wafugaji.
Alisema ng'ombe wanaotakiwa katika Wilaya hiyo ni wale waliosajiliwa na kwa sasa Mifugo yote iliyokamatwa itapigwa faini ila kuna zoezi jipya litafanyika hivi karibuni na Mifugo yote itakayokamatwa wahusika watafikishwa mahakamani na Mifugo kupigwa mnada.
Amewataka wafugaji wote wilayani humo kuheshimu sheria za kuwa na Mifugo michache inayotambulika na kutoingiza Mifugo mingine ili kulinda Bonde la MTO Kilombero ambalo linatazamwa na taifa kama tegemeo la mradi Mkubwa Wa uzalishaji umeme katika mto Rufiji(Stigles gorge).
Akizungumzia kuhusu wakulima na wafugaji kutumia eneo la Bonde oevu,Ihunyo alisema msimu Wa Kilimo umeisha na yakishatolewa mazao wakulima na wafugaji hawatakiwi kuonekana tena katika maeneo hayo.
Kwa upande wake Meneja Wa poritengefu la Kilombero Linus Chuwa alisema kumekuwa na tatizo la muda mrefu la uvamizi Wa eneo hilo na wameanzisha zoezi la kuwaondoa wavamizi katika Wilaya ya Malinyi na sasa Kilombero na kutakuwa na doria endelevu lengo ni kuondoa Mifugo yote katika Bonde hilo.
Nae mmoja Wa wafugaji aliyekamatwa na Mifugo yake Chimagale Mtema alisema wanaheshimu maamuzi ya serikali ila alioeleka Mifugo yake katika Mashamba ya wakulima baada ya kuona wakulima wametoa mazao yao ila ameiomba serikali kuwatengea maeneo ya kulishia na kunyweshea Mifugo yao na hii itasaidia kutoingia maeneo ya wakulima.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa