Pichani juu: Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa akikagua Mradi wa ujenzi wa Hospitli ya Wilaya hiyo.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa mapema jana ametembelelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mlimba iliyopo pembezoni mwa makao makuu ya wilaya hiyo.
Akiwa katika ziara za ukaguzi wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo wilayani humo,Mhandisi Kaliwa, amemtaka mkandarasi wa hospitali hiyo kuendana na muda kuhakikisha ujenzi huo unaisha kwa wakati kwani hadi sasa serikali imekuwa ikisisitiza kutekelezwa kwa miradi mingi ambayo inahitaji kumaliziwa ikiwemo ujenzi wa hospitali hiyo
Aidha mhandisi Kaliwa alipongeza jitihada zinazoendelea kufanywa na mkandarasi huyo licha ya changamoto wanazo pitia katika kuhakikisha wanakamilsha ujenzi wa hospitali hiyo ambayo itakuja kukupunguza mzigo mkubwa wa huduma za afya Wilayani humo.
Hata hivyo Mhandisi Kaliwa amewaomba wananchi wanaoishi kuzunguka maeneo hayo kuhakikisha wanaendelea kutoa ushirikiano kwa mkandarasi wa hospitali hiyo hasa katika kipindi ambacho suala la nguvu kazi linahitajika.
Ujenzi wa hospitali ya wilaya kwa sasa upo katika hatua ya Linta, umegharimu kiasi cha shilingi milioni Mia Tano (500,000,000/=) ambapo ulianza mapema mwezi Julai mwaka huu na unatarajiwa kukamilika ifikapo mapema mwezi Disemba 2020.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa