Na, Milka Kaswamila-Mlimba DC
Mkurugenzi Mktendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mlimba, ndg. Jamary Idrisa Abdul, mwishoni mwa wiki iliyopita aliongoza kikao cha Kamati ya Lishe, ya Halmashauri hiyo, cha kujadili bajeti ya awali ya huduma za Lishe kwa ajili ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Kupitia Kikao hicho, Mkurugenzi Jamary alisema, kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri inakwenda kutenga fedha shilingi milioni 97 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za Lishe huku makadirio kwa ajili ya kila mtoto yakiwa ni shilingi 1,800 kutoka shilingi 1,700 ya mwaka wa fedha unao endelea hivi sasa.
Naye Afisa Lishe wa Mkoa wa Morogoro, ndg. Salome Magembe, ambaye alikuwa miongoni mwa wajumbe walioshiriki kikao hicho ameitaka Halmashauri kuhakikisha bajeti wanayoiandaa inaakisi vipaumbele vya mkoa wa Morogoro vya utekelezaji wa shughuli za Lishe ili kuweza kufikia malengo tazamiwa kimkoa na kitaifa kwa ujumla.
Pia, Afisa huyo ameitaka Halmashauri kuhakikisha taarifa za utekelezaji wa afua za Lishe zinazotolewa ni halisia kwa sababu suala la Lishe ni miongoni mwa vipaumbele ya Taifa hivyo taarifa zisipokuwa na uhalisia zinaweza kupelekea Halmashauri kukosa wadau ambao huenda wangeweza kujitokeza kufadhili maeneo yenye mapungufu kwa manufaa ya jamii husika, Halmashauri na Taifa kwa ujumla.
Kwa sasa, Halmashauri ya Wilaya Mlimba inakadiriwa kuwa na jumla ya watoto 54,436 wenye umri wa chini ya miaka mitano, kundi muhimu sana ambalo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuhakikisha haliwi na udumavu wala utapiamlo.
Makundi mengine ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, vijana wa umri wa balehe, wajazito na wanawake wanao nyonyesha.
MWISHO
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa