Halmashauri ya wilaya ya Mlimba imeamua kupeleka pesa kwenye miradi mikubwa na yenye tija tu ili kuweza kuharakisha upatikanaji wa maendeleo kwa wananchi.
Akizungumza na muandishi wa habari hii, mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba mhandisi Stephano Kaliwa amesema kuwa, wameamua kuachana na miradi midogo midogo kwanza na kufikiria kupeleka pesa kwenye miradi mikubwa na yenye tija tu ili kuweza kuharakisha maendeleo kwa wananchi.
Akiitaja miradi hiyo mikubwa Mhandisi Kaliwa amesema miradi kama shule za kidato cha sita za bweni, madarasa, miradi ya umwagiliaji, Mradi wa kutengeneza matofali ili kurahisisha ujenzi wa haraka wa nyumba za wananchi na hata ofisi na vituo vya afya ndio miradi pekee itakayoweza kupata pesa nyingi kwa kipindi hiki ili kuweza kurahisisha maendeleo.
Nae mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba Mhandisi Baraka Lolila amesema kuwa tayari wamekwishajipanga kuhakikisha kuwa miradi tajwa hapo juu inafikia malengo yake kwa sababu kila kitu kinachohitajika kwenye kukamilisha hayo kipo tayari, pesa zipo tunasubiri taratibu tu za kiserikali kukamilika ili tuweze kuanza kazi, kuhusu utengenezaji wa matofali tayari tumekwishanunua mashine ya Kufyatua tofari hizo na tumekwishaanza kufyatua tofali zimeanza kufanya kazi kadhaa kwa maendeleo.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa