TUMEWASIKIA NA TUMEWAFIKIA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Eng. Stephano B. Kaliwa ameeleza mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika Mkutano wa Vyombo vya Habari uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkoa wa Morogoro Novemba 2, 2023.
Akibainisha hayo Eng. Stephano B. Kaliwa amesema kuwa katika sekta za Afya, Elimu, Maji na Miundombinu, wameweza kupunguza na kutatua changamoto mbalimbali za Wananchi
Hata hivyo katika sekta ya Afya Serikali imewezesha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya yenye thamani ya Shilingi 3,014,000,000, vituo vya Afya katika kata ya Uchindile, Chita, Igima, mofu na Utengule, Zahanati tisa na vifaa tiba katika Hospital ya Wilaya, vituo vya Afya na zahanati pamoja na ujenzi wa nyumba ya mtumishi 3 kwa 1 na kupelekea upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa ufanisi.
Sambamba na hayo katika sekta ya Elimu Msingi imeboreshwa kwa kujengewa shule 15 mpya na shule 3 zitasajiliwa mwaka huu. Ujenzi wa bweni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum shule ya Msingi Ngajengwa, uendelezaji wa miradi ya Boost na shule uboreshaji wa shule Kongwe pamoja na ujenzi wa shule ya mchepuo wa kingereza.
Aidha kwa upande wa Elimu Sekondari imejengwa shule ya Msingi Ihenga, Merera, Miembeni Girls, Matema, Chiwachiwa, na shule ya Sekondari mpya kata ya Mngeta.
Faida za Miradi ya Elimu imesaidia kuondoa Utoro kwa wanafunzi, kutembea umbali mrefu kupata huduma za kielimu na kuondoa adha ya walimu kukosa makazi.
Mafanikio Mengine kwa ya Kilimo, uendelezaji wa shamba la korosho katika kata ya Kamwene jumla ya ekari 135 zinalimwa pamoja na kilimo cha maparachichi 8,878 kata ya Uchindile na shamba la Miti ekari 2500.
Katika sekta ya Maji, miradi mikubwa imejengwa na inaendelea kutekelezwa katika kata ya Mbingu, Mlimba, Uchindile, Chita(Merera/Idunda) , na Namwawala (Kisegese)
Mkutano huo umehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Wakuu wa Wilaya za Morogoro, Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro ukiwa na lengo la utekelezaji wa Kampeni ya kutangaza mafanikio ya Serikali kwa miaka mitatu iliyozinduliwa Novemba 1, 2023 Jijini Dodoma.
*Mlimba right destination for investment*
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa