Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Bw. Jamal Idrisa Abdul amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa msaada wa mahitaji kwa waathirika wa mafuriko katika kata ya Masagati pamoja na waliokumbwa na changamoto ya rrli ya TAZARA kufunikwa na kifusi katika kata ya Kamwene kijiji cha Lumumwe.
Mkurugenzi amemshukuru Mhe. Rais kwa kuleta ndege mbili, zilizotumika katika kuokoa na kufanya tathimini ya Uharibifu wa nyumba na mzao pamoja na kuwaletea tani 4 za chakula kwa waathirika hao wa Mafuriko.
Aidha. Wananchi wamemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Upendo na faraja yake katika kipindi hiki kigumu kwao
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa