pichani juu: Dkt Charles Tizeba (mwenye skafu ya bendera ya Tanzania)akimsikiliza kwa makini mtaalam wa halmashauri (Hayupo pichani) akizungumzia namna Halmashauri ya wilaya ya kilombero walivyofanikiwa kudhibiti Tembo kwa kutumia Nyuki.
Mapema leo Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba amewataka wataalam wa nyuki wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero kuungana nae kwenye safari ya simiyu kwaajili ya kwenda kutoa mafunzo ya namna ya kuzuia Tembo kwa kutumia Nyuki, kwenye kilele cha sikukuu ya Nanenane kitaifa inayofanyika kwenye mkoa huo.
Akizungumza huku akiwa na furaha sana alipotembelea banda la maonyesho ya kilimo la Halmashauri ya wilaya ya kilombero, lililopo maeneo ya Nanenne Morogoro mjini, Dkt Tizeba amesema kuwa amefurahishwa sana na teknolojia hiyo ambayo ni nyepesi sana isiyokuwa na gharama na yenye faida kubwa sana kwa wakulima, n kwakuw imeanzia kilombero basi anahitaji wataalam wa kilombero waende huko Simiyu wakaambukize teknolojia hiyo.
Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero ndg Dennis Londo, amesema kuwa, amelipokea agizo hilo kwa mikono miwili na analifanyia kazi, na tayari ameagiza wataalam hao wakiwemo mkulima mmoja wa nyuki toka kikundi cha Njokomoni, cha mang’ula, mtaalam aliyeshirikiana na mkulima huyo kutengeneza mizinga hiyo na wafadhili wa mradi huo wa shirika la AWF.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa