Aliyekuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli mapema jana amefariki dunia katika Hospitali ya Mzena iliyopo maeneo ya Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Taarifa hiyo ya Msiba imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ambapo amesema kuwa Marehemu alipelekwa katika hospitali ya Jakaya mrisho Kikwete kwa shida ya Umeme wa Moyo ambapo alitolewa na kurudi katika shughuli zake kabla ya kuzidiwa ten ana kukimbizwa katika hospitali ya Mzena ambapo ilipotimu majira ya saa kumi na moja jioni siku ya Tarehe 17/03/2021 aliaga Dunia.
Dr Magufuli atakumbukwa kwa umahiri wake wa kutimiza matakwa yake kwa vitendo kwani tayari alikuwa katika mikakati mizuri ya kuiunganisha Tanzania kwa barabara za lami, alifanikiwa kuihamisha Tanzania na Kuipeleka Dodoma huku akisimamia vyema ulipaji wa kodi uliopelekea kununua ndege kadhaa za serikali hali iliyopelekea kufufua shirika la ndege la Tanzania, huku akisisitiza watu kufanya kazi kwa bidi na kujifunga mkanda kwaajili ya maendeleo ya watanzania wote hasa wale masikini.
Alihakikisha kila wilaya inajenga Hospitali zake huku akifufua bwawa la umeme la mwalimu Nyerere ambapo awali lilijulikana kama Stiglers Gorge, alifanikiwa pia kurudisha heshima ya madini kwa kuweza kufanikisha mikataba iliyopelekea Tanzania kupata faida kubwa sana tofauti na awali huku akifanikiwa kujenga ukuta mkubwa kule Mirerani Arusha ambapo ilikuwa ni maalum kwa kuzuia utoroshwaji wa madini huku kila mkoa ambao ulikuwa na madini ulijengewa soko kubwa la madini na mabo mengine mengi aliyoyafanya hayataweza kusahaulika.
Bwana Ametoa, na bwana ametwaa,
Jina lake lihimidiwe,
Mwanga wa milele umpe eee bwana,
Apumzike kwa amani,
AMINA
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Dokta John Pombe Joseph Magufuli, Mahali pema Peponi.
AAMIYN.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa