Kupitia agizo la Waziri wa nchi, ofisi ya Raisi, Tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe. Seleman S. Jafo la kuzitaka Halmashauri 31 ambazo ofisi zake zipo nje ya maeneo yao ya utawala kwa kipindi cha siku 30 kuanzia tarehe 07.10.2019 ziwe zimehamishia ofisi zao kwenda katika maeneo yao ya utawala.
Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Kilombero limeridhia kwa pamoja kuhamishia makao makuu ya wilaya ya Kilombero kutoka Ifakara kwenda Tarafa ya Mngeta.
Akitangaza uamuzi huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero Mh. Daudi Ligazio kupitia kikao maalum cha baraza la madiwani katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero mapema leo tarehe 15.10.2019 kuwa kupitia agizo la Mh. Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli tumeamua Kuhamishia makao makuu ya wilaya ya Kilombero kwenda Tarafa ya Mngeta.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa