Halmashaui ya wilaya ya Kirombero Mkoani Morogoro, imekutanisha wadau wote wa maendeleo kujadili mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo, ili kuboresha na kufanya maendeleo yazidi kukuwa kwa kasi na kuwa mazuri zaidi katika jamii.
Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo Mjini Ifakara, ambapo umetoa nafasi kwa wadau wote wa maendeleo, kuelezea taasisi zao kwa jinsi zinavyofanya kazi kuhusiana na masuala mazima ya maendeleo.
Aidha Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Kilombero ,imeahidi kushirikiana kikamilifu na wadau hao wa maendeleo, kwa mambo mbalimbali wanayoyafanya katika taasisi zao, ili kuendelea kukuza maendeleo katika hali ya haraka zaidi.
Lakini pia wadau hao wa maendeleo, wameshauriwa kuzungumzia masuala ya lishe zaidi, pindi wanapokutana na wananchi kupitia taasisi zao, na ikiwezekana kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo, atafutwe mtaalam wa mambo ya afya, ili kuelezea kwa undani zaidi masuala ya lishe kama vile umuhimu wa lishe na athali zitokanazo na kutotumia lishe.
Ushauri huo umetolewa mara baada ya tafiti zinazoonesha kwa asilimia thelathini na tatu ya watoto wanaoishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, wanasumbuliwa na tatizo la utapia mlo, na hii ni kutokana na kutokuwa na matumizi sahihi ya lishe.
Hata hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero pamoja na wadau wote wa maendeleo Wilayani humo, wamekubaliana wawe wanakutana mara mbili kwa mwaka ikiwezekana mwezi wa sita na mwezi wa kumi na mbili ili kuendelea kujadili mambo mengi zaidi yanayohusu maendeleo.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa