• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MLIMBA DISTRICT COUNCIL
MLIMBA DISTRICT COUNCIL

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA MLIMBA

  • Mwanzo
  • kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/ Asili
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
      • Muonekano wa muundo
    • Idara/ Vitengo
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango, Takwimu na ushirika
      • Mazingira na Usafi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Maji
      • Ardhi, Maliasili na Mazingira
      • Ufugaji na uvuvi
      • CHF iliyoboreshwa
      • Sheria
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Msingi
      • Sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za watumishi
    • Rasilimali watu
    • TEHAMA
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha, utawala na mipango
      • Elimu, Afya na maji
      • Uchumi, Ujenzi na mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Kumuona mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha
      • PICHA ZA MIRADI YA MAPAMBANO DHINI YA UVICO

Halmashauri ya wilaya ya Kilombero yapima ardhi, yatoa hati za umiliki

Posted on: June 18th, 2018

Pichani mkuu wa wilaya ya kilombero ndg James Ihunyo.

VIPANDE vya ardhi 60,430 vimepimwa kwa wananchi katika vijiji 30 wilayani Kilombero ikiwa ni utekelezaji wa Programu ya Kuwawezesha Umilikishaji Ardhi(LTSP)inayosimamiwa na Wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi.

Hayo yamebainika wakati wa utoaji wa hati miliki za kimila 1030 kwa wananchi wa kijiji cha Mpanga kata ya Kisawasawa mapema juzi ambapo makamishna wa ardhi kutoka katika kanda zote nchini walihudhuria.

Mkuu Wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika makabidhiano hayo aliishukuru wizara ya Ardhi kwa kuleta Mpango huo katika wilaya yake na Wilaya Jirani za Ulanga na Malinyi na kuwataka wananchi kutambua thamani ya Ardhi wanazomiliki.

Ihunyo alisema vijiji 80 vitapimwa katika Mpango huo na hadi sasa vijiji 30 vimeshapimwa na wao kama Wilaya watahakikisha wanasimamia kikamilifu zoezi hilo kabla ya kumalizika mwakani huku akiwatahadharisha wanaopenda kuzalisha migogoro waache Mara moja.

Aidha Mkuu huyo Wa Wilaya ameiomba serikali kuangalia utaratibu mpya Wa kuyaunganisha mabaraza yote kuanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya kuwa wizara moja tofauti na sasa ambapo mabaraza ya kijiji na kata yapo wizara ya Tamisemi huku la Wilaya likiwa wizara ya Ardhi na kwa kufanya hivyo ufanisi utakuwepo katika mabaraza hayo.

Kwa upande wake kamishna Wa Ardhi Mary Makondo aliwataka wananchi waliopimiwa vipande vyao vya Ardhi kwenda katika ofisi na kuchukua hati zao kwani hawatatozwa kodi yoyote kabla na baada ya kuchukua hati hizo tokana na hatimiliki za kimila kutotozwa kodi yoyote na serikali.

Makondo aliwashangaa wananchi Wa kijiji cha Mpanga kusuasua kusaini hati zao kwani Mashamba 2999 yamepimwa huku yakusainiwa ni 1300 tu na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo kwani haitojirudia na zoezi likiisha mwakani litaenda katika Wilaya nyingine.

Nao wananchi waliopata hatimiliki za kimila wameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza ahadi zake kwa wakati na vitendo baada ya kuwapimia maeneo yao na kuwapatia hati miliki za kimila bila gharama yoyote.

Walisema kuwa wakati mradi unaanza waliambiwa zoezi litachukua miaka mitatu na wananchi wote kupata hati miliki na kweli zoezi hilo limefanyika kwa ukamilifu na sasa wananchi wengi wana hati kabla ya zoezi hilo kumalizika mwakani.

 ā€¯Tunamshukuru Rais wetu na watendaji wake kwa kutujali wananchi Wa chini na kutupatia huduma muhimu bure kama hili la hati miliki za kimila,hivyo tunategemea kumaliza kabisa migogoro ya Ardhi katika maeneo yetu,"alisema Mohamed Shukuru.

Nae Husna Kidali alisema zoezi la kuwapimia na kuwapatia hati wanawake litasaidia kuondoa mfumo dume Wa kumiliki Ardhi kwani baada ya kuwapa elimu kila kaya iliridhia kugawana Sawa vipande vya Ardhi bila kujali kuwa ni ya mume ama mke.

Programu ya LTSP inatekelezwa katika wilaya tatu za Kilombero,Ulanga na Malinyi katika mkoa Wa Morogoro ambapo pamoja na kuwapimia na kuwapa hatimiliki wananchi pia hutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe katika mabaraza ya Ardhi ya vijiji na kata katika Wilaya hizo lengo ni kumaliza kabisa tatizo la migogoro ya Ardhi.
 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI February 24, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2023 December 14, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MATUMIZI YA KAWAIDA JULAI 2022 August 01, 2022
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MLIMBA IMEPOKEA PESA ZA MATUMIZI YA KAWAIDA KUTOKA HAZINA (OC) KWA MWEZI NOVEMBA 2022 TSHS 35,294,000/= December 05, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI

    August 07, 2023
  • MAADHIMISHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI

    August 07, 2023
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MATUMIZI YA KAWAIDA KUTOKA HAZINA (OC) TSH. 235,360,000.00

    August 02, 2023
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MATUMIZI YA KAWAIDA KUTOKA HAZINA (OC) TSH. 235,360,000.00

    August 02, 2023
  • Angalia zote

Video

MHE. WAKILI DUNSTANI KYOBYA AHAIDI TSH. 500,000.00/= KWA KILA MWANAFUNZI ATAKAYEPATA DIVISHENI 1.7.
video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Fomu ya maombi ya ruhusa
  • Fomu ya utambulisho benki
  • Fomu ya Kuhuisha Uanachama CHF iliyoboreshwa
  • Wasifu wa Wilaya
  • Muundo wa Halmashauri
  • Eneo la Kijiografia
  • Fursa za Uwekezaji Kilombero

Viunganishi linganifu

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Idara kuu ya Takwimu (NBS)
  • Tovuti kuu ya Takwimu huria

kitafutio cha watembeleaji wa duniani

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Mngeta Kijiji cha Itongoa

    Anuani: P.O.BOX 263

    Simu: 023 293 1523

    Mobile: 0232931523

    Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa