Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba imekabidhi hundi ya Sh Milioni 500 kwa vikundi 44 vya Wanawake na Watu wenye Ulemavu pamoja na Pikipiki 52 zenye thamani ya TSh Milioni 135 kwa vikundi 44 vya vijana katika kutoka kata ya Masagati, Mlimba, Ching’anda, Mngeta na Idete . Fedha hizo ni mikopo inayotokana na asilimia 10 inayotolewaga na Serikali kwa makundi hayo matatu.
"Miezi mitano nyuma Halmashauri, ilikabidhi Tsh Milioni 918 na Pikipiki 20 kwa vikundi vya Wanawake, watu wenye ulemavu na Vijana amesema Kaimu Mkurugenzi Bi Witness Kimoleta, kipindi hiki tunakabidhi Tsh Milioni 516 na Pikipiki 52 zenye thamani ya Tsh Milioni 135, kwetu hii ni hatua kubwa sana ya kuzidi kuyainua makundi haya matatu kwa kuhakikisha yananufaika na mikopo hii isiyo na riba inayotolewa na Serikali kupitia Halmashauri zetu.
Niwaombe Ndugu zangu mliopata mikopo hii, nendeni mkaifanyie kazi vizuri ili muweze kulipa marejesho yenu bila usumbufu, kwa kufanya kazi kwa bidii mtakua mmemuunga mkono Rais Samia ambaye Serikali yake ndio inayotoa mikopo hii isiyo na riba.
Wito umetolewa kwa maafisa Biashara, Maafisa Ugani kutembelea vikundi hivi mara kwa mara ili kutoa ushauri wa kitaalamu waweze kufanya biashara zao vizuri, tusikae ofisini tu tusaidieni kuwafuata hawa wajasiriamali wanaopata mikopo hii na kuwapa elimu. Pia, watendaji kata wamesisitizwa kuvisimamia na kuvishauri vikundi hivyo
Halmashauri itahakikisha wanaweka miundombinu bora kwa vikundi vinavyokidhi vigezo kuweza kupatiwa mikopo hiyo huku akiwaasa kuirudisha kwa muda waliopangiwa ili wengine wenye sifa waweze kupatiwa mikopo hiyo.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa