Pichani juu: Moja ya Kamera zilizofungwa kwenye majengo ya Halmashauri.
Katika kuongeza ulinzi katika Halmashauri ya wilaya ya Mlimba, uongozi ueamua kufunga kamera katika kila kiunga cha Halmashauri hiyo.Akizungumza na mwandishi wa Habari hii, Afisa TEHAMA wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba ndg Rashid Ligaya amesema kuwa, halmashauri hiyo imeamua kutumia mbinu hiyo kutokana na ukweli kuwa, hiyo ndio njia pekee ya kutambua kila aina ya uhalifu ambao unaweza kutokea katika eneo la Halmashauri.Pmaoja na hayo yote ndg Ligaya amesisitiza kuwa njia hii ni salama na haraka unaweza kutambua kila aina ya usumbufu kwani unaweza kuingia hata kwa kutumia simu kwenye mtandao wa kamera hizo popote pale utakapokuwepo kwani inahitaji mtandao wa Internet tu.Nae mlinzi wa Halmashauri hiyo ndugu Nasoro amesema kuwa wanaishukuru Halmashauri kwa kuweza kufunga Kamera hizo kwani kwa wao ni ukombozi
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa