Siku ya Tarehe 26/2/2018 ilikuwa ni siku ya huzuni sana kwa wakaazi wa kijiji cha Namwawala, Wafanyakazi wa
Halmashauri ya wilaya ya kilombero, wananchi, ndugu, jamaa na marafiki kutokana na kumhifadhi ndugu yetu
mpendwa aliyekuwa Diwani wa kata ya Namwawala aliyezikwa huko nyumbani kwao Namwawala.
Akizungumza na wananchi na wanafamilia, mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero
ndugu Dennis Londo amesema kuwa msiba wa diwani huyo umewasikitisha sana sio tu kwasababu
amefariki ila ni namna gani alivyofariki.
''kwakweli kifo cha mheshimiwa Lwena kimeacha pengo, na kimetusikitisha sio tu kwasababu amefari
bali namna alivyofariki, bila shaka ni majonzi ambayo hayatakuwa na namna ya kufutika'' Alisema.
Aidha kwa upande mwingine alisema kuwa kama Halmashauri wamejitahidi kwa namna walivyoweza
kuhakikisha kuwa wanampatia stahili zote za kuhitimisha mazishi hayo ikiwamo kugharamia jeneza,
usafiri na mambo yote ambayo yalifanikisha shughuli hiyo.
Mwisho alisisitiza kwa namna ya kuwaomba wananchi wa eneo hilo kuhakikisha kuwa wanayaendeleza
yale mazuri yote ambayo marehemu aliyaacha kwanialikuwa ni mtu muadilifu na alikuwa mfano wa kuigwa
na mcghapakazi mno na mwenye kupenda wananchi wa kata yake, lakini pia hakuna kitu cha kuwafariji
zaidi ya kuwapa pole, poleni sana wananchi wa kata ya Namwawala, alimaliza.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa