Pichani juu mheshimiwa Rais John Magufuli akikata utepe pamoja na baadhi ya wafadhili na viongozi wengine, kuashiria kufunguliwa kwa ujenzi wa barabara ya Kidatu - Ifakara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli mwishoni mwa wiki hii ameweka jiwe la Msingi la ujenzi wa barabara ya Kidatu – Ifakara hapa Wilayani Kilombero itakayojengwa kwa kiwango cha lami ambayo ina urefu wa kilometa 66.9.
Aidha, Rais Magufuli amewataka wananchi wa Maeneo ambayo barabara hiyo inapita kutoa ushirikiano wa dhati kwa Mkandarasi wa kampuni ya Renolds Construction Company Ltd yenye makao yake makuu nchini Nigeria wanaojenga barabara hiyo ili aweze kukamilisha barabara hiyo kwa wakati na kwa kiwango kinachohitajika.
Amesema Barabara hiyo ambayo ujenzi wake utakamilika mwaka 2020, ni muhimu kwa sababu ni kiunganishi cha barabra kuu ya TANZAM kuanzia Mikumi - Kidatu – Ifakara – Mahenge hadi pori la akiba la Selous.
Akizungumza zaidi kwenye hutuba yake Rais Magufuli amesema kuwa, barabara hiyo ni kiunganishi cha barabara kuu ya ukanda wa kusini ya Mtwara – Mingoyo – Masasi – Tunduru – Songea – Mbinga hadi Mbamba Bay. Hivyo itarahisisha usafiri na usafirishaji wa Mazao na mali ghafi kutoka na kwenda katika bonde la mto Kilombero hususan Wilaya za Kilosa, Kilombero, Malinyi na Ulanga.,
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbawala amesema kuwa Mkandarasi wa barabara tayari yuko eneo la ujenzi, kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa asilimia mia moja.
Barabara hii hadi kukamilika kwake itagharimu kiasi cha shilingi za kitanzania 104.914 bil. ikiwa ni ufadhili wa Umoja wa nchi za Ulaya zilizotoa asilimia 49.15 ya gharama ya ujenzi huo, Uingereza 40.13% USAID 10.72 na gharama iliyobaki italipwa na Serikali ya Tanzania.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa