Mkuu wa wilya ya Kilombero na mwenyekiti wa kikao cha kamati ya sheria cha mwaka wa fedha 2019/2020 Ndugu James Ihunyo amewataka wakuu wa idara mbalimbali katika halmashauri kusimamia kwa umakini miradi iliyopo na kubuni miradi mipya ili kuongeza mapato ya halmashauri.
Hayo amezungumza katika kikao cha kamati ya ushauri cha wilaya tarehe 26/1/2019 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya kilombero cha kupitia mpango na bajeti ya halmashauri wa wilaya mwaka wa fedha 2019/2020. Amesema kipato hicho kitasaidia matumizi mengine wakati wa utekelezeji wa shughuli mbalimbali ndani ya halmashauri.
Katika bajeti hiyo Ihunyo amesema mazao ya kokoa na mpunga ni vyanzo vikuu ya pato la halmashauri japo kutopewa kipaumbele katika kuimarisha uzalishaji wake”nimeamua kulisemea hili kwasababu ni zao ambalo linafanya vizuri,niombe idara ya kilimo itazamwe upya katika bajeti hii na ninyi maofisa hakikisheni mnatoa elimu ya kutosha kwa wakulima ili wazalishe kwa kiasi kikubwa zao hili tupate mapato ya ziada”amesema Ihunyo
Kikao hicho ni maususi kwa lengo la kupitia na kushauri makadilio ya bajeti ya mwaka 2019/2020 kwa halmashauri ya wilaya ya Kilombero ambacho kimeshirikisha maafisa wa sekretariti mbalimbali,viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wa dini,wajumbe toka sekta mbalimbali na wadau wa maendeleo.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa