Pichani juu: Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa (mwenye koti jeusi) akijadiliana jambo na Afisa manunuzi Ndg Ezekiel Bernad
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mlimba Injinia Stephano Kaliwa mapema leo amekagua baadhi ya vifaa vya ujenzi wa ofisi mpya ya Halmashauri ya wilaya ya Mlimba pamoja na Hospitali ya wilaya ya Mlimba na kusema kuwa maendeleo ni mazuri.
Akizungumza na Afisa manunuzi wa Halmashauri hiyo ndg Ezekiel Bernad, amesema kuwa vifaa hivi ni muhimu sana kuhakikisha kuwa vinahifadhiwa vizuri ili vitumike kwa utaratibu uliopangwa.
Katika mazungumzo yake ameshauri kamati zote zihakikishe zinashirikiana ipasavyo ili kufanya shughuli hii ya ujenzi wa majengo hayo uende kwa haraka na kwa utarabu utakaoiwezesha Halmashauri kunufaika na si kupata Hasara.
Nae Afisa manunuzi ndg Bernad amesema kuwa kwakuwa wanakamati wote kwa kamati zote wapo, hivyo watakaa na kujadiliana namna bora ya kuendesha shughuli hiyo ili kufanya kama walivyoelekezwa na mkurugenzi.
‘’kwa kuwa wanakati wote wapo kwa kamati zote za ujenzi wa majengo hayo wapo hivyo basi tutakaa leo na kuhakikisha tunaweza mikakatio thabiti katika kufanikisha ujenzi huo kwa mujibu wa taratibu za serikali zinavyotaka.’’ Alisema afisa Manunuzi Bernad.
Habari picha
Baadhi ya vifaa vya ujenzi pamoja na madawati ambayo mkurugenzi alikagua mapema asubuhi ya leo
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa