Pichani bi Niindaeli Malugu akionyesha kadi hiyo ambayo husaidia watoto kupata huduma ya chanjo popote walipo.
je unaijua kadi ya saratani ya mlango wa kizazi?
mratibu wa afya wa halmashauri ya wilaya ya kilombero bi Niindaeli Malugu amesema kuwa kadi ya chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ni kadi ambayo hutumika katika kutambulisha watoto wote ambao wamekwishachanjwa kwaajili ya kupata huduma hiyo kokote watakapokuwa nchini Tanzania.
Bi Malugu aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake, alipotaka kujua umuhimu wa kadi hizo kwa watoto hao wadogo ambao wana umri wa miaka 14, ambao kwao imeonekana kuwa wapo katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo ikiwa hakutakuwa na hatua za haraka za kuwasaidia hazijachukuliwa.
Akitoa ufafanuzi zaidi bi Malugu alisema kuwa kuna uwezekano kuwa baada ya mtoto kupewa chanjo hiyo leo, basi baada ya miezi sita ikatokea yupo Dar es salaam kwa shangazi yake hivyo, ataweza kupata chanjo hiyo ambayo huitajika kurudiwa kila baada ya miezi sita akiwa huko alipo muhimu aionyeshe kadi hiyo hapo itakuwa rahisi kwake kuweza kupata hudum hiyo.
Aidha alisisitiza kwa wazazi kuwaruhusu watoto wao kuweza kupata chanjo hiyo, kwani ni muhimu sana kwaajili ya afya zao kwa siku za baadae, na hazina madhara yoyote na kuwa watoto wote ambao wamekwishapata chanjo hiyo wanaendelea na masomo yao kama kawaida, alimaliza.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa