KAMATI YA TAMISEMI YARIDHISHWA NA MRADI WA BOOST HALMASHAURI YA WILAYA YA MLIMBA.
Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imefanya ukaguzi wa Mradi wa kuboresha Elimu ya Msingi (Boost) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba shule ya Msingi Igima kata ya Igima kwa kukagua Ujenzi wa Madarasa ya mradi huo.
Mhe. Dennis Londo Mwenyekiti wa Kamati ya TAMISEMI ameipongeza Menejimenti na Watumishi wa Halmashauri kwa kusimama kwa ueledi na ubora mradi wa Boost kwa shule ya Msingi Igima na kusema Mradi unaakisi thamani halisi ya fedha iliyotolewa. Aidha, Mhe. Dennis Londo ametoa Maagizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Wakili Dunstan Kyobya kuhakikisha anashgulikia suala la Kivuko cha TAZARA ili kurahisisha njia ya wanafunzi kwenda Shuleni bila kuathiriwa na changamoto hiyo.
Pili, ameuagiza uongozi wa Halmashauri kuhakikisha shule inaendelea kutunzwa na kuwa katika Mazingira safi ya kutolea huduma ya kielimu.
Mradi huu wa Boost umegharimu Jumla ya kiasi cha shilingi Milioni mia nne sabini na tano na laki tatu, kwa kujenga vyumba vya madarasa 16, vyumba 2 vya madarasa ya Elimu ya awali, Jengo moja la Utawala na matundu ya Vyoo 28 vya wanafunzi pamoja na walimu.
Shule ya Msingi Igima ina Jumla wanafunzi 1023 ambapo (Me 484 Ke 539) walimu 10 (Ke 5, Me 5)
Mhe. Justine Nyamoga (MB. Kilolo) amewashauri wazazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwa suala la lishe mashuleni na kuhakikisha wazazi/ walezi wanapeleka vyakula shuleni ili wanafunzi wapate mahitaji ya chakula wakiwa shuleni kusaidia kutopoteza vipindi shuleni, amesisitiza zaidi kuzingatia lishe bora kwa wanafunzi hao.
Pia Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi amewapongeza walimu wa shule ya Msingi kwa usimamizi mzuri wa Miradi ya Boost na kuomba eneo la vyoo vya wanafunzi wawekewe vioo ili kumfanya mwanafunzi kuendelea kuwa nadhifu. Pamoja na hivyo Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi ameeleza umuhimu wa kujengwa kwa Bwawa la Mwalimi nyerere ni Kuzuia mafuriko ya mto rufiji, kuzalisha Umeme, kilimo cha Umwagiliaji na Mwisho ni kutunza Mazingira.
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa