Mapema leo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya kilombero ikishirikiana na viongozi kadhaa wa halmashauri ya wilaya ya kilomberoimetembelea familia ya aliyekuwa Diwani wa kata ya namwawala marehemu Godfrey Luena kwaajili ya kutoa salamu za rambirambi na kuwafariji wafiwa kutokana na msiba huo.
Akizungumza na wafiwa pamoja na wananchi wa kijiji hicho cha Namwawala, mwenyekiti wa kamati hiyo ya ulinzi na usalama ya wilayaambae pia ni mkuu wa wilaya ya kilombero mheshimiwa James Ihunyo alisema kuwa serikali imesikitishwa sana na kitendo hicho kibaya kilichofanywa na watu ambao walikuwa na nia ya kujichukulia sheria mkononi, alisisitiza kuwa serikali inakilaani kitendo hicho kwa nguvu kubwa huku akiomba ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi ili kuhakikisha watu wote waliofanya kitendo hicho wanachukuliwa hatua za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo.
Nae kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya kilombero ndugu Mohammed Ramadhani alitilia mkazo suala hilo na kusema kuwa halmashauri imesikitishwa sana na kitendo hicho na hivyo kuwasihi sana wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu wanachopitia katika kufanikisha kumhifadhi ndugu yetu bwana Luena, pamoja na yote hayo bwana Ramadhani alisisitiza kuwa Halmashauri itakuwa bega kwa bega na familia hii mpaka pale marehemu Luena atakapohifadhiwa katika nyumba yake ya milele.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Daudi Ligazio alikiri kuwa amempoteza kiongozi muadilifu na shupavu katika baraza lake la madiwani, huku akionekana kushindwa kujizuia kwa majonzi alisema kuwa hakika pengo lake halitazibika, na kuwa kama baraza watamkumbuka sana kutokana na hoja zake na namna alivyo shupavu katika kusimamia hoja alizoziamini.
Kwa upande wa familia akitoa ratiba ya msiba huo baba wa marehemu ndg Joakim Luena alisema kuwa, anaishukuru sana kamati ya ulinzi na usalama na uongozi mzima wa halmashauri ya wilaya ya kilombero kwa kuja kumzika Ndg Luena, lakini pia alitanabaisha kuwa mazishi ya mwanae yatafanyika tarehe 27/2/2018 siku ya jumanne, katika meeneo ya kijiji hicho cha Namwawala, kinachosubiriwa kwa sasa ni ndugu zake na pindi watakapofika tu basi taratibu zote za maziko zitafuatwa.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE, AMINA
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa