Na, Milka Kaswamila-Mlimba DC
Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Kilombero, leo tarehe 03.01.2025, imekagua miradi ya maendeleo ambayo inatazamiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu katika Halmashauri ya Wilaya Mlimba.
Katika ziara hiyo jumla ya miradi saba ya sekta za afya, elimu, maji, maendeleo ya jamii, utawala na barabara imekaguliwa na ushauri mbalimbali umetolewa ili kuhakikisha inakuwa na ubora unao takikana.
Halmashauri ya Wilaya Mlimba mwaka huu inatazamia kupokea Mwenge wa Uhuru tarehe 16.04 kutoka Halmashauri ya Wilaya Malinyi.
MWISHO
Mngeta Kijiji cha Itongoa
Anuani: P.O.BOX 263
Simu: 023 293 1523
Mobile: 0232931523
Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa